Na
Clief Mlelwa,Makambako
Halmashauri
ya mji wa Makambako mkoani Njombe imepokea vifaa vya kujikinga na homa kali ya
mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara
mjini humo vyenye thamani ya milioni moja laki saba na elfu sitini na tano.
Akizungumza
wakati akipokea vifaa hivyo mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa makambako Hanana
Mfikwa amewashukuru wafanyabiashara hao kwa kutoa vifaa hivyo na kueleza kuwa
jamii inatakiwa kuungana kwa pamoja katika kukabiliana na janga hili la corona
badala ya kuiachia serikali ama watu wachache.
Mganga
mkuu wa halmashauri ya mji wa Makambako Alexndaer Mchone amesema kuwa
atahakikisha vifaa hivyo vinatumika sehemu husika na amewataka wananchi
kuendelea kuchukua tahadhili kwa kuepukana na mikusanyiko isiyo ya lazima na
kutoa taarifa pindi wanapo pokea wageni kutoka kwenye maeneo ambayo
yameathirika na corona.
Naye
mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe Siphael Msigala amesema
kuwa wafanyabiashara ambao wametoa vifaa hivyo kwa awamu ya kwanza ni wale
wafanyabiashara wa soko kuu la mazao na wale wenye milango stendi ya zamani na
baadhi yao ambao wapo nje ya soko hilo.
Hata
hivyo mwenyekiti wa soko kuu Makambako Bwanakijiji Sanga na mwenyekiti wa stendi ya zamani Nasa Kyando
wamesema kuwa wameamua kuchangia vifaa hivyo ili kukabiliana na virusi vya
Corona
0 Comments