TANGAZA NASI

header ads

Jonijoo akacha Wasafi Media, atimkia E FM Radio na TV E



Mtangazaji Jonijoo ambaye alikuwa anafanya kazi Wasafi FM na Wasafi TV ameondoka kwenye vituo hivyo na kujiunga na E FM na TV E Tanzania.

Mkurugenzi wa E FM na TV E , Francis Ciza maarufu kama Majizzo ndiye amemtambulisha mtangazaji huyo pendwa miongoni mwa vijana wengi kwenye familia yake.

“Jonijooo unasema mitaa imekulea, Naomba Nikukaribishe kwetu Waswahili Tuliotumwa na mtaa, Natambua uwezo wako, njoo Tulisongeshe,” amesema Majizzo na kuendelea.

“Mimi CEO wa Waswahili nikupe tu taarifa kwamba Hatuna Shughuli ndogo. Kuanzia leo @efmtanzania na @tvetanzania ndio familia yako. Karibu sana,” ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ikumbukwe ndani wa Wasafi Media, Jonijoo alifanya vipindi viwili ambavyo ni Block 89 upande wa Redio, na The Bartender upande wa TV.
#Chanzo:bongoswaggz

Post a Comment

0 Comments