Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia pamoja na vifaa vya kutengenezea noti hizo.

Mtuhumiwa alikamatwa  mnamo tarehe 11.04.2020 majira ya saa 00:30 usiku huko eneo la sokoni, kata ya Kyela kati,tarafa ya Unyakyusa, wilaya ya Kyela, mkoa wa Mbeya.

Jeshi la Polisi mkoani hapo lilimkamata JOHN FRANCIS [22] mfanyabiashara na mkazi wa Olofea – Kyela akiwa na noti bandia dola za kimarekani 09 kila noti sawa na dola 100 kama zingekuwa halali sawa na dola 900.

Zikiwa na Na. LB399120505B, noti za Zambia Kwacha 40 kila noti sawa na noti za Zambia kwacha 100 kama zingekuwa halali sawa na kwacha 4,000. kati ya noti 20 zina Na. EH122082777 na noti nyingine 20 zina Na. EH122082854