Msanii wa muziki bongo,Maua Sama ameweka wazi anapokuwa kwenye mahusiano na mwanaume kila mmoja huwa anajitegemea kifedha lakini haimaanishi kuwa akipewa hatopokea.
Kauli hiyo inakuja mara baada ya hivi karibuni kuweka wazi anatafuta mchumba mwenye mapenzi ya kweli, huku akisisitiza ahitaji fedha za mchumba huyo.
“Wanaume wote ambao wameshakuwa na mimi, pesa zake zinakuwa za kwake na zangu zinakuwa za kwangu. Sisemi kuwa mimi sitaki pesa au pesa ni ngumu, ukinipa napokea, mwanaume akitokea kama ana mapenzi, tunakuwa sawa,” Maua Sama ameiambia Wasafi TV.
Hata hivyo Maua Sama ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Nioneshe, amesema mpenzi aliyenaye kwa sasa amekuwa akimsadia sana kifedha
0 Comments