TANGAZA NASI

header ads

Davido azidi kuunga mkono jitihada za kupambana na Corona




Davido ni mmoja wa mastaa ambao wapo mstari wa mbele kwenye kupigana vita dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona
Star wa Muziki wa nchini Nigeria amefungua mfuko maalumu wa mapato yote yatakayopatikana kwenye video yake mpya "Dolce & Gabba" iliyotoka ijumaa iliyopita kwenda kusaidia kwenye utafiti dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.


Kampuni ya Dolce & Gabbana ilianzisha mfuko wa kuchangia fedha kukiwezesha Chuo Kikuu cha Humanitans cha nchini Italia kufanya Utafiti dhidi ya virusi vya Corona, hivyo mapato hayo ya Video ya Davido yatakwenda moja kwa moja kwenye mfuko huo.

Kwenye mahojiano hayo na CNN, Davido pia ameweka wazi kwamba familia yake kwa ujumla wametoa mifuko 6,000 ya mchele kusaidia chakula kwenye jimbo lao la Osun vilevile kwa Ujumla Familia yake imetoa kiasi cha zaidi ya TSH. Bilioni 3 (USD 1.3 million) kwa serikali kupambana na Corona.

Wiki chache zilizopita mchumba wake, Chioma alithibitishwa kukutwa na maambukizi ya Corona lakini kwasasa tayari ameshapona.

Post a Comment

0 Comments