Na Bilgither Nyoni,Makambako
Wazazi na walezi wametakiwa kuwalinda watoto wao Kwa kuwahakikisha wanawazuia kucheza pamoja na kuzurula ovyo ili wasiweze kupata homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.
Hayo yamesemwa na kaimu afisa elimu msingi katika halmashauri ya mji wa Makambako BHOKE BIRORE wakati akizungumza na Ice fm Ofisi kwake ambapo amesema mzazi au mlezi analo jukumu la kumlinda mtoto wake ili asipate maambukizi hayo hususani katika kipindi hiki cha likizo.
Aidha Birore amepiga marufuku walimu kuanzisha vituo vya kufundisha masomo ya ziada(Tuition) baada ya shule kufungwa kwa agizo la waziri mkuu Majaliwa Kasimu na kusema kuwa kwa wale watakaokaidi hatua kazi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo Birore Amewataka wazazi au walezi kuhakikisha wanawasaidia watoto wao hasa wadogo kuwafundisha au kuwanunulia vitabu ili waweze kujisomea katika kipindi hiki cha likizo.
Nao baadhi ya wazazi pamoja na wanafunzi mjini Makambako wamesema wamesema kutokana na ongezeko la wagonjwa wa Covid-19 wataendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali.
0 Comments