TANGAZA NASI

header ads

Ubalozi wa Sweden waahidi kuendeleza uhuru wa habari na kujieleza nchini

 



Na Amiri Kilagalila,Njombe


Ubaraozi wa Sweden Nchini Tanzania umeahidi kuendelea kuungana na watanzania wote katika jitihada za kukuza na na kuendeleza uhuru wa habari na kujieleza hapa nchini.


Hayo yamebainishwa na balozi wa Sweden hapa nchini Bw,Anders Sjoberg hii leo wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine Duniani katika kuadhimisha siku ya uhuru wa habari na kujieleza.



Bw,Anders Sjoberg amesema nchi ya Sweden inaamini manedeleo ya nchi yeyote yanaweza kupatikana kwa kupeana taaarifa,kujadiliana kwa uwazi na uwajibikaji hivyo wapo tayari katika kuendeleza jitihada hizo.


“Basi sisi tutaendelea kuungana na watanzania wote katika jitihada za kukuza na kuendeleza uhuru wa habari na kujieleza nchini”alisema Bw,Anders Sjoberg


Aidha amesema Tanzania na Sweden ni marafiki hivyo nchi zote mbili zinatambua umuhimu wa nguzo hii.


“Sweden na Tanzana ni marafiki wa siku nyingi na wote tunatambua nguzo hii,sambamba na haki ya kupata taarifa ni muhimu sana kwa jamii inayoheshimu demokrasia na haki za binadamu”alisema Anders Sjoberg



Vile vile amesema anafurahi kuwepo nchini Tanzania na kuungana katika madhimisho ya siku ya uhuru wa habari.


“Mimi kama balozi wa Sweden ninafurahi sana kuwepo leo kusheherekea uhuru wa habari na kujieleza”alisema 


Mei 3 kila mwaka nchi ya Tanzania huungana na mataifa yote duniani katika kuadhimisha siku ya uhuru wa habari na kujieleza ambapo hii leo kauli mbiu inasema “Habari kwa manufaa ya umma”



Post a Comment

0 Comments