TANGAZA NASI

header ads

Diamond Platnumz alamba dili Warner music awachana Forbes " Mnifatilie vizuri kujua utajiri wangu kabla ya kuniweka kwenye orodha ya kipumbavu"




 Msanii Diamond Platnumz amesainishwa mkataba na kampuni ya kimataifa ya @warnermusic inayofanya kazi na wasanii wakubwa ulimwenguni kama Cardi B, Bruno Mars, Charlieputh, Burna Boy n.k

Hii ni hatua kubwa kwa Diamond Platnumz kwani itamfanya kuwa na urahisi wa kufanya kazi na wasanii zaidi ya 50 ambao wote wanafanya kazi chini ya mwamvuli wa @warnermusic.

Taarifa ya Diamond Platnumz kuingia mkataba na Warner Music imethibitishwa pia kupitia ukurasa wa Mziiki hapa Instagram.

Katika hatua nyingine mkali huyo amewachana Forbes na kuwataka kumfuatilia vizuri utajiri wake kabla hawajamuweka kwenye orodha isiyo na mashiko ya wasanii matajiri Afrika.

"Forbes, wakati mwengine munifuatilie vizuri (google) kujua utajiri wangu kabla ya kuniweka kwenye orodha ya kipumbavu ya wasanii matajri zaidi Afrika" - @diamondplatnumz ameandika.

Hii imekuja baada ya tovuti ya Nigeria kuandika kuwa, #Diamond ametajwa na jarida la Forbes kama msanii namba 28 tajiri zaidi barani Afrika akiwa anamiliki utajiri wa dola za Kimarekani Milioni 5 jambo ambalo mashabiki wengi wa mkali huuoy walilipinga kutokana na namba hizo kuwa ndogo ukilinganisha na thamani na uwekezaji alioufanya.

Post a Comment

0 Comments