Watu saba wamefariki nchini Uingereza kutokana na damu kuganda mwilini baada ya kupewa chanjo ya Oxford-AstraZeneca, mamlaka ya kudhibiti dawa imethibitishia BBC.
Kwa ujumla wato 30 kati ya milioni 18 waliopewa chanjo hiyo kufikia Machi 24 wamekabiliwa na hali ya damu kuganda.
Bado haijulikani ikiwa ni bahati mbaya tu au athari ya kweli ya chanjo.
Shirika la udhibiti wa Dawa na Bidhaa za Afya linanasema faida ya chanjo zinaendelea kuzidi madhara yake.
Hata hivyo, hali ya kuganda kwa damu kwenye ubongo, kitaalamu "cerebral venous sinus thrombosis" au CVSTs zimesababisha nchi nyingine - zikiwemo Ujerumani, Ufaransa na Canada - kudhibiti utumizi wa chanjo hiyo.
Shirika la Afya duniani na Wakala wa Dawa wa Ulaya wanasema faida za chanjo hiyo huzidi hatari zozote.
Data zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa (MHRA) siku ya Ijumaa, zilionesha kuwa watu 22 walipata hali ambayo kwa lugha ya kimatibabu inafahamika kama cerebral venous sinus thrombosis (CVST) ambayo ni aina fulani ya mgando wa damu kwenye ubongo.
Hii ilifuatiwa na na viwango vya chini vya seli, zinazosaidia damu kuganda, mwilini. MHRA pia ilibaini watwengine wanane walikabiliwana tatizo la damu kuganda mwilini.
Sasa MHRA imethibitishia BBC kupita barua pepe, kwamba "inasikitika watu saba wamefariki ".
Dkt June Raine, Afisa mkuu mtendaji wa MHRA, amesema: "Manufaa… ya kudhibiti maambukizi ya Covid-19 na changamoto zake yanaendelea kuwa juu kuliko hataru yoyote kwa hiyo watu wakubali kupewa chanjo wakiombwa kufanya hivyo."
Uchunguzi wa kubaini ikiwa chanjo ya AstraZeneca inasababisha hali isiyokuwa ya kawaida ya damu kuganda mwilini, inaendelea.
Mapema wiki hii Shirika la Dawa la Muungano wa Ulaya lilisema "halijathibitisha, lakini kuna uwezekano".
Hatari inaweza kuwa kubwa kiasi gani?
Inabaki uwezekano kabisa kuwa hatari haipo kwani chanjo hazijathibitishwa kusababisha kuganda kwa damu kwenye ubongo.
Taasisi ya Paul Ehrlich ya Ujerumani imeripoti visa 31 na vifo tisa kati ya watu milioni 2.7 waliopewa chanjo huko.
Hatahivyo, data za hivi karibuni za Uingereza ziliripoti visa vitano tu, kati ya watu zaidi ya milioni 11 waliopewa chanjo.
Shirika la Dawa la Ulaya, ambalo limetathmini data kutoka kote ulimwenguni, linakadiria kuwa kuna hatari moja kati ya 100,000 ya CVST kwa watu walio chini ya umri wa miaka 60 ambao wamepewa chanjo ya AstraZeneca.
Mkuu wa ufuatiliaji wa usalama wa shirika hilo, Dk Peter Arlett, alisema hiyo ni "zaidi ya tunavyotarajia kuona".
Hatahivyo, haijulikani ni kweli kiasi gani kuhusu kiwango cha hali hii kujitokeza kwenye ubongo hapo kabla. Makadirio yanatofautiana kutoka kwa karibu kesi mbili kwa watu milioni kila mwaka hadi karibu 16 katika kila watu milioni kwa nyakati za janga la corona yenyewe inaweza kuwa inasababisha pia.
Chanjo ya AstraZeneca ni salama?
Hakuna usalama kwa asilimia mia moja katika dawa na hata tiba ambazo ni hatari hutumiwa katika mazingira yanayofaa.
Dawa za tiba ya mionzi zina athari mbaya, lakini zina thamani kubwa; na hata dawa za kutuliza maumivu kama paracetamol na ibuprofen zina athari mbaya, ni nadra sana.
Uamuzi huegemea kwa kutazama faida zinazozidi hatari.
Hii ni changamoto haswa katika janga la corona. Kawaida dawa inategemea "kanuni ya tahadhari" kuthibitisha usalama wa kutosha kabla ya kutoa dawa mpya kwa idadi kubwa ya watu. Lakini katika janga hilo, ucheleweshaji wowote wa chanjo ya watu pia utagharimu maisha.
Kulingana na data ya Ujerumani peke yake, ikiwa chanjo ya watu milioni moja basi unatarajia watu 12 watakuwa na tatizo la damu kuganda na wengine wanne watakufa.
Lakini ikiwa watu milioni wenye umri wa miaka 60 watapata virusibasi karibu 20,000 watakufa na Covid-19. Ikiwa watoto milioni 40 wa miaka wanapata virusi hivyo basi karibu 1,000 hufa. Ingekuwa watu mia chache katika miaka yao ya 30.
Faida za chanjo huongezeka kwa kutegemea umri na nchi kama Ujerumani na Canada zimeruhusu chanjo ya AstraZeneca kutumika katika vikundi vya wazee. Uamuzi huu pia utasababishwa na chanjo mbadala ambazo zinapatikana na ni nani bado anahitaji kupatiwa chanjo.
Ulimwengu unachunguza data kwa nguvu, lakini majibu yatachukua muda.
0 Comments