TANGAZA NASI

header ads

Songwe wakoshwa na ujenzi wa vyoo bora Njombe,waahidi kufanya makubwa

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Timu ya watu 55 ikiongozwa na mkuu wa mkoa  wa Songwe brigedia Nicodemas Mwangela imehitimisha ziara ya siku tatu wilayani Njombe ya mafunzo kwa vitendo ya utekelezaji wa kampeni ya usafi wa mazingira na ujenzi wa vyoo bora na vya kisasa ambayo haifanyi vyema katika mkoa huo ulionzishwa mwaka 2016.

Shabaha ya ujio wa timu hiyo mkoani Njombe ni kujifunza mbinu zilizotumiwa na timu nzima ya utekelezaji wa kampeni hiyo pamoja na wananchi na kuifanya halmashauri ya wilaya ya Njombe kuendelea kuwa kinara katika mashindano ya kitaifa mfururizo katika utekelezaji wa kampeni ya maji na usafi wa mazingira.

Wakizungumza mara baada ya kutembelea vijiji tofauti vya halmashauri ya wilaya ya Njombe na kisha kuelezwa njia walizotumia kufikia mafanikio katika utekelezaji,viongozi na watalaamu wa idara ya afya mkoa wa Songwe akiwemo Samwel Opulukwa ambaye ni mkuu wa wilaya ya Songwe,Dkt Seif Shakalage na Dkt Hamad Nyembea ambaye ni mganga mkuu wa mkoa wa Songwe wanasema ni kupunguza mabavu na badala yake elimu na makubaliano ndiyo yamefanya wakazi wa Njombe kujenga vyoo bora kwa hiari.

Kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Songwe,katibu tawala wa mkoa huo Dkt, Seif Shakalage amewahakikishia UNICEF pamoja na mkoa wa Njombe utayari wao wa kwenda kutekezeza zoezi hilo kikamilifu ili kuufikia mkoa wa Njombe.

“Katika mkoa wa Songwe watu kuwa na vyoo tuna asilimia 99.6%  kwa hiyo tunapokuja kujifunza hapa ni kwajili ya kumalizia kazi yetu,mimi ninayo timu nzuri kwa hiyo tunaenda kumalizia kazi iliyobaki”alisema Shekalage

Aidha amewashukuru viongozi wa mkoa wa Njombe kwa ushirikiano waliouonyesha katika kuwajengea uwezo wa zoezi hilo lililoleta mafanikio wilaya ya Njombe.

Naye katibu tawala wa mkoa wa Njombe Katarina Revocat kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe,amewaomba shirika la UNICEF wafadhili wa mradi wa utekelezaji wa zoezi la usafi wa mazingira kuongeza wigo wa maeneo ya utekelezaji wa mradi zaidi ya wilaya mbili kama ilivyo sasa ukilinganisha na mkoa wa Songwe unakotekelezwa mkoa wote.

“Tunawaomba UNICEF mtengeneze uwanja sawa,mkoa wa Songwe unakwenda kama mkoa mzima lakini Njombe mnasapoti wilaya mbili hapa mtusaidie kidogo”alisema Revocat

Aidha amepongeza mkoa wa Songwe kwa ujasili wa kujitoa na kuja kujifunza katika mkoa wa Njombe huku akiwashukuru wataalamu wa mkoa wa Njomnbe walioshiriki na kusadia kutoa elimu kwa wageni hao.

“Nawashukuru sana ndugu zangu wa Njombe kuweza kupokea wageni,mpaka sasa hivi wanaondoka wakiwa wanakumbuka ile huduma mliyoitoa hongereni sana”alisema Revocat

Frenk Odhiambo ni mkuu wa kitengo cha maji na usafi wa Mazingira kutoka UNICEF amesema anatarajia mafanikio makubwa kutoka mkoa wa Songwe kutokana na ushirikianao wao huku akiadi kwa niaba ya shirika kuwa bega kwa bega na serikali ya Tanzania katika kuendeleza shughuli zinazofanywa na shirika ili kuisadia jamii ya watanzania.

Idadi kubwa ya vyoo  vya kaya za mkoa wa Songwe Vipo daraja A na B ambayo si bora kiafya huku Njombe hususani katika halmashauri ya wilaya ya Njombe vikiwa katika ngazi  ya juu na salama kiafya ambayo C na D.

Post a Comment

0 Comments