TANGAZA NASI

header ads

Waziri atoa onyo kwa watumishi wa afya

 


Serikali imeonya tabia ya baadhi ya watoa huduma za afya wanaotoa lugha za matusi na kejeli kwa wagonjwa kuacha mara moja ama sivyo, watapoteza ajira.


Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Godwin Mollel, aliyekuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya zamani mjini Sengerema.


Onyo hilo la Dk Mollel limetokana na kilio cha wananchi waliomweleza kwamba, baadhi ya watoa huduma wamekuwa na lugha chafu kwa wagonjwa na kuwafanya wengi kukata tamaa kwenda kutibiwa kwenye hospitali za Serikali.


Mmoja wa wananchi hao Anastazia Simon, amesema baadhi wa watoa huduma za afya wamekuwa kero kwa wagonjwa kutokana na lugha chafu na kelei wanazokutana nazo.


“Mimi ni mhanga wa matusi na kejeli za watoa huduma, nilimpeleka mzazi wangu Hospitali ya Wilaya kwa lengo la kupatiwa matibabu, lakini nilikutana na matusi,” alimweleza Dk Mollel.


Kutokana na kilio hicho cha wananchi, Dk Mollel amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Sengerema kusimamia nidhamu ya watumishi wa afya wanapotoa huduma ya kwenye vituo.

Post a Comment

0 Comments