Na Gabriel Kilamlya,Njombe
Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe
mkoani Njombe Lauteri Kanoni amewataka wananchi kupunguza ulevi huku akizuia
kutolewa kwa vibali vya matamasha ya burudani[disko] katika kipindi hiki cha
maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli.
Marufuku hiyo ameitoa
akiwa kata ya Igwachanya katika mkutano wa maombolezo ya msiba wa na kwamba
kitendo cha kufanya matamasha ya burudani na ulevi wa kupindukia havitavumiliwa
katika kipindi hiki cha siku 21 za maomboleza ya msiba wa kitaifa.
"Itatushangaza sana tunalia kilio kikubwa
hivi halafu watu kwenye baa wanapiga 'Ndomboloo ya Solo' inamaana wewe hauko
pamoja na sisi Naelekeza tupiga nyimbo za maombolezo na tupunguze ulevi, Hakuna vibali vya disco vitakavyotolewa kwa kipindi hiki
tutakuwa tumekiuka taratibu"Alisema Dc Kanoni
Awali katibu tawala wa
wilaya ya Wanging'ombe Edward Manga amesema kuwa mchango wa Magufuli katika
taifa hili umekuwa wa kuigwa barani Afrika kwani amefanikiwa kuifikisha nchi
katika uchumi wa kati kabla ya wakati uliopangwa.
Mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Agnetha Mpangile amesema pigo
lililowakuta watanzania la kuondokewa na Rais Magufuli halitosahaulika huku
viongozi wa dini akiwemo Mbaraka Thabiti Sheikh wa wilaya hiyo wakisema
watanzania hatupaswi kukata tamaa kwani maandiko yanasema baada ya kifo cha
mussa alitumwa Joshua kwenda kuwafikisha wana wa Israel kwenye nchi ya ahadi.
Baadhi ya wakazi wa Wanging'ombe
akiwemo Aiden Valanzi na Erasto Homange wamesema kifo cha Magufuli kimewagusa
sana kwa kuwa aliwatetea sana wanyonge.


0 Comments