TANGAZA NASI

header ads

RC NDIKILO ATOA MIEZI MITATU KWA MAFUBILO KUWALIPA WAKULIMA WA KOROSHO DENI LA MIL.356

 


Na MWAMVUA MWINYI,PWANI


MKUU  wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa miezi mitatu kwa ,mmiliki wa Kampuni ya Mafubilo General Supplies  iliyopo Kibaha kuwalipa wakulima wa korosho deni wanalodai la zaidi ya sh.milioni. 356.156.3.

Fedha hizo wanadai wakulima wa Kibaha baada ya korosho zao  kilo 282,306.5  zilizokuwa kwenye  vyama vya ushirika (Amcos) vitano kuuzwa kwa  Kampuni hiyo.

Ndikilo alitoa agizo hilo ,Mjini Kibaha wakati wa kikao maalum  na wakulima ambao waliingiia mkataba na muwekezaji  huyo. 

Aidha ,alimpa muda huo kuhakikisha analipa deni hilo na akishindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mkuu huyo wa Mkoa ,alielekeza mmiliki wa Kampuni hiyo kulipa fedha hizo kwa awamu tatu kila awamu ahakikishe analipa kwa awamu milioni milion 118.

Pamoja na hilo, alitoa muda mfupi kwa muwekezaji huyo kukiri kuwa atalipa deni hilo pindi atakapopata barua ya kumtaka alipe.

Kwa mujibu wa mkataba uliosainiwa mwezi Februari, mwaka 2020 kati ya Kampuni ya Mafubilo na vyama hivyo vya ushirika ni kwamba mnunuzi alitakiwa kulipa fedha hizo kwa muda wa siku 63.

Amcos zilizoshiriki kusaini mkataba huo ni Kongowe ( kilo 168,982.50), Mwendapole (kilo 2,279) na Misugusugu (kilo 72,314), Visiga (kilo 36,244) na Mkombozi ( kilo 2,487) na kwamba kilo zote za Korosho zina thamani ya Shilingi 394,156,335.30 hadi sasa ni Shilingi Milion 40 tu ambazo zimelipwa na Kampuni hiyo.

Wakulima hao walieleza,wamekuwa wakisumbuka kwa muda mrefu kufatilia jambo hilo na kwamba  sasa wameanza kuona muelekeo wa kupata haki zao.

Post a Comment

0 Comments