Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella awaonya watendaji wa halmashauri kuacha kufuata miongozo ya wizara badala yake waangalie uhitaji wa wananchi ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mongella alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua kikao cha mapendekezo na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na kuongeza kuwa muongozo wa wizara pekee hautoshi kukidhi uhitaji katika maeneo husika.
Alisema baadhi ya wanaoandaa miongozo hiyo hajawahi kukaa hata ngazi ya kijiji, kata, au halmashauri, wanawezaje kuelekeza ujenzi wa vyumba vya madarasa matano huku uhitaji ukiwa ni madarasa zaidi ya hayo.
"Achaneni na miongozo hiyo wewe unaweza kuelekeza halmashauri kujenga madarasa matano ili kuweka nini, kuku, miongozo ya kijinga hiyo wewe ukijenga madarasa matano hapo watoto utawaweka wapi, nyumbani kwako, kwa maana hiyo tukiweka madarasa matano kwa halmashauri tayari mtajitosheleza? halafu unasema ndiyo muongozo haiwezekani hiyo," alisema Mongella.
0 Comments