TANGAZA NASI

header ads

Makamu mtawala wa Dubai afariki dunia

 


Waziri wa fedha wa Umoja wa falme za kiarabu na pia makamu mtawala wa Dubai,Sheikh Hamdan bin Rashid Al Maktoum amefariki dunia.T

angazo la kifo chake limetolewa leo Jumatano na mtawala wa Dubai kupitia ujumbe wa Twitta. Sheikh Hamdan alikuwa na umri wa miaka 75 na alikuwa ni kaka wa mtawala wa sasa wa Dubai,Sheikh Mohammed bin Rashid al-Makhtoum.

Ofisi ya habari ya serikali ya Dubai,imesema kwamba ibada ya kumswalia itahudhuriwa na watu wa familia tu kutokana na janga la virusi vya Corona. 

Utawala wa Dubai umetangaza siku 10 za maombolezo ambapo bendera zote zitapeperushwa nusu mlingoti kuanzia leo Jumatano na taasisi zote za serikali zitafungwa kwa siku tatu kuanzia kesho Alhamisi.

Post a Comment

0 Comments