TANGAZA NASI

header ads

Diwani na askari sungusungu wanadaiwa kufyatuliwa risasi na Mfanyabiashara

 


Diwani wa Kata ya Miembeni katika Manispaa ya Moshi  na Askari (Sungusungu) wanadaiwa kufyatuliwa risasi na Mfanyabiashara mmoja mkoani Kilimanjaro wakati wakifanya ulinzi shirikishi usiku, baada ya kukuta Watu wakiwa wanafanya mapenzi Barabarani.

Diwani huyo anasema waliwakuta Watu hao wanafanya mapenzi Barabarani karibu na eneo la Bar na wakati wanahojiana nao akatokea Mfanyabiashara ambaye pia ni Mmiliki wa Bar hiyo na kuwazuia kitendo kilichopelekea vurugu hadi akafyatua risasi na kumjeruhi Askari mmoja.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro Ronald Makona amethibitisha kutokea kwa taarifa hizo na kusema wanamshikilia Mfanyabiashara huyo na muda wowote atafikishwa Mahakamani.

Post a Comment

0 Comments