Uchaguzi wa bunge uliofanyika nchini Ivory Coast mnamo Machi 6 ulitamatishwa kwa ushindi wa chama tawala cha Rally of Houphouëtists for Democracy and Peace (RHDP).
Kulingana na matokeo ya mwisho yaliyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini Ivory Coast, chama cha RHDP cha Rais Alassane Ouattara kilipata viti 137 katika bunge lenye jumla ya wanachama 255, na kufikisha idadi nyingi zaidi.
Katika nchi hiyo iliyokuwa na wapiga kura takriban milioni 7, kiwango cha ushiriki katika zoezi la uchaguzi kilikuwa asilimia 37.
Ouattara, ambaye alishinda uchaguzi wa urais nchini humo mnamo Oktoba 2020, aliingia madarakani kuongoza kwa muhula wake wa tatu.
0 Comments