TANGAZA NASI

header ads

Canada yataka nchi iwakilishwe na Rais badala ya Malkia

 


Katika nchi ya Canada ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola ya Mataifa ya Uingereza, takriban nusu ya watu wameitaka nchi yao iwakilishwe na rais atakayechaguliwa badala ya Malkia wa Uingereza.


Asilimia 45 ya wananchi wa Canada walioshiriki mchakato ulioandaliwa na wakala wa utafiti wa kura ya maoni, walibainishwa kwamba wanapendelea kuwa na rais wa nchi aliyechaguliwa kuliko Malkia.


Ilielezwa kuwa pendekezo hili lilikuwa "katika kiwango cha kihistoria" ambapo limeongezeka kwa alama 13 zaidi ikilinganishwa na utafiti kama huo uliofanywa na wakala hao mnamo Februari 2020.


Wakati asilimia 24 ya wahojiwa walionekana kupendelea Canada ibaki ya kifalme, asilimia 18 walisema "hawakujali hata kidogo juu ya suala hili" na asilimia 13 walikosa maamuzi.


Maoni ya kupambana na ufalme, ambayo yaliongezeka hadi asilimia 51 kati ya wanaume wenye umri wa miaka 35-54, yalifikia asilimia 57 kati ya wakaazi wa mkoa wa Quebec, wanaojulikana kwa maoni yao ya kujitenga.


Asilimia 31 ya wahojiwa walisema nchi hiyo itakuwa na rais aliyechaguliwa katika miaka 20 ijayo.


Watu walioshiriki utafiti huo pia walisema kwamba chaguo la kwanza la mrithi wa Malkia Elizabeth II atakapofariki, ni Prince William.


Wakati asilimia 35 ya watu wakionekana kutaka kumwona Prince William kwenye kiti cha enzi kama Mfalme wa Uingereza, asilimia 22 yao walitoa maoni ya kumpendelea Prince Charles.

Post a Comment

0 Comments