TANGAZA NASI

header ads

Wakuu wa shule wekeni vifaa vya tahadhari vya majanga ya moto Weibina

 


Na Timothy Itembe Mara.

Wakuu wa shule za sekondari mkoani Mara wamejadili jinsi  ya kujikinga na majanga ya moto mashuleni.

Akitoe elimu hiyo mbele ya wakuu wa shule za sekondari mkoani hapa,kaimu kamanda jeshi la zima moto na uokoaji wilaya Tarime,CPL Siraji Rashidi Ayubu alisema kuwa majanga ya moto ni moja ya janga baya linalosababisha hasara kwa serikali na jamii kwa ujumla.

“Jamii na wakuu wa shule wanatakiwa kuwa na elimu ya majanga ya moto  pia jamii na wakuu wa shule inatakiwa kuwa na vifaa vya  kuzimia moto kwenye shule kama Fire Extingusha pamoja na kushirikisha wanafunzi elimu ya zima moto”alisema Ayubu.

Ayubu aliongeza kuwa ukaguzi wa system ya vifaa vya moto unatakiwa,kutumia vifaa vilivyopo kuzima moto,kuzima main swith ya umeme,kupiga simu kwa haraka kwa kutumia namba 114 pamoja na kufanya uokozi alipo mtu.

Naye mkuu wa shule ya sekondari Kenyamanyori,Zefania Jolijo alisema kuwa majanga ya moto ni moja ya majanga ambayo yanalitia hasara Taifa pamoja na jamii kwa ujumla kwa kughamia hasara ya kufidia vifaa na majengo yaliyoteketea kwa moto kwa hali hiyo  kuna haja jamii kupata elimu ya kujikinga na majanga ya moto.

Mkuu huyo aliongeza kusema kuwa majanga ya moto yanaondoa utulivu wa wanafunzi wawapo shuleni na hawasomi kwa raha ambapo wanakuwa na wasiwasi mashuleni nyakati za masomo usiku.

Jolijo aliwataka wanafunzi kuepuka baadhi ya vifaa vinavyosababisha majanga ya moto kama vile kuingia na simu kuchaji ndani ya mabweni kuepuka kutumia Hita za maji pamoja na vifaa vingine ambavyo vinaweza kusababisha majanga ya moto.

Afisa elimu taaluma mkoani hapa,Zacharia Weibina  ambaye alikaimu nafasi ya Afisa elimu mkoani hapa ambaye alialikwa kama mgeni rasimi bila kuhudhuria kwa sababu za kiserikali  katika kufunga semina hiyo iliyokuwa ikiwendeshwa kwa wakuu wa shule za sekondari mkoani Mara ya siku moja alisema kuwa kuna haja elimu ya majanga ya moto kutolewa kila wakati ili kujiepusha na majanga ya moto mashuleni.

Afisa huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa shule kutumia lugha rafiki kwa jamii pamoja na wanafunzi huku akijua kuwa lengo la serikali nikutaka kuwa na kizazi chenye mwamko wa maendeleo na wala siovinginevyo.

Weibina aliwaomba wakuu wa shule kuhakikisha kila shule inakuwa nha vifa vya kuzimoa moto ili kujikinga na majanga ya moto ya mara kwa mara mashuleni ambayo yanasababisha hasara kwa serikali na kwa jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake Ambilinyi Ayubu ambaye ni afisa elmu taaluma mkoani hapa aliwataka wakuu wa shule kwenda na kuhamasisha zoezi la kukimbia mchakamchaka mashuleni huku akiwataka kutunga nyimbo ambazo zinahamasisha uzalendo.

Post a Comment

0 Comments