Na Allawi Kaboyo – Bukoba.
Umoja wa wanawake Tanzania Mkoa wa
Kagera katika kuadhimisha miaka 44 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wamefanya mambo mbalimbali ndani ya Manispaa ya Bukoba ikiwemo kupatiwa elimu
ya afya kuhusu salatani ya mlango wa kizazi pamoja na lishe bora.
Warsha hiyo imefanyika kaika viwanja vya
kituo cha afya Zamuzamu kilichopo kata ya Bilele feburuari 01,mwaka huu, na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wa mkoa na wilaya huku mgeni
rasmi akiwa ni katibu mwenezi wa chama hicho Ndg. Hamimu Mahamudu.
Akitoa elimu kwa wanawake waliohudhuria
warsha hiyo kuhusu salatani ya mlango wa kizazi Bi Dunia ameeleza kuwa watu
walio hatalini kuambukizwa au kupata ugonjwa huu ni wasichana walioanza kufanya
ngono kwa umri mdogo, mwanamke mwenye wanaume wengi kwa wakati mmoja, mwanamke
anayevuta sigara na mwanamke mwenye maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Dunia ameongeza kuwa salatani hiyo
inatibika hivyo wanawake wanatakiwa kujenga tabia ya kupima mara kwa mara kwa
kuwa dalili zake hazionekani haraka japo madhara yake ni makubwa pale
inapochelewa kutibiwa.
Kwaupande wake mtaalamu wa lishe
kwaniaba ya afisa lishe manispaa ya bukoba amesema kuwa watoto wengi wamekuwa
wakizaliwa wakiwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya udumavu, lishe duni
kutokana na mama zao kutozingatia mlo kamili.
Ameonngeza kuwa tatizo la udumavu na
lishe duni kwa watoto limekuwa sugu hasa kwa ukandaa huu wa
Kagera hali inayopelekea kuwepo kwa namba kubwa ya watoto wenye udumavu na
kuwashauri wanawake kuzingatia aina za vyakula wanavyotakiwa kula wakati wa
ujauzito na baada ya kujifungua ili kumjengea mtoto afya njema.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo katibu
mwenezi wa ccm Kagera Hamimu Mahamudu ameishukuru jumuiya hiyo kwa kuadhimisha
kuzaliwa kwa chama chama chao kwa kuwapa wanawake elimu hasa inayo husu afya ya
mama na motto maana kundi hilo ndilo linalotegemewa.
Amewataka wanawake waliopata elimu hiyo
kuwa mabalozi wema kwa wanawake wengine kwa kuwapa elimu waliyoipata huku
akiagiza vikao vyote vya chama hicho kwa ngazi zote kuweka agenda ya lishe.
“Ninakushukuru mwenyeki wa UWT kwa jambo
hili, huwezi kuwaongoza wanachama au wananchi wakiwa hawana afya, kwa mantiki
hiyo kama msemaji wa chama wa Mkoa huu naagiza kwenye vikao vyenu na vya chama
kuanzia ngazi ya shina hadi mkoa kuwepo na agenda ya lishe” Amesema
Mahamudu.
Hamimu ameupongeza uongozi wa kituo cha
afya Zamuzamu kwa usimamizi mzuri ambao umepelekea kituo hicho
kuboreshwa na kuwa na wodi kubwa ya wazazi, chumba cha upasuaji, maabara ya
kisasa na miundombinu iliyoimara huku kikiongeza idadi ya wattumishi kutoka
watumishi 28 hadi 51 waliopo sasa.
Bi Anna Kajuna ni mwenyekiti wa
UWT Wilaya ya Bukoba mjini ambaye ameeleza mambo waliyoyafanya kituoni hapo
ikiwemo elimu ya afya, upimaji wa salatani ya mlango wa kizazi, utoaji wa damu
na ukaguzi wa miundombinu ya kituo hicho.
Mama Kajuna amewataka wanawake
kuzingatia elimu waliyopata huku akiwataka kujenga tabia ya kupima afya hali
itakayowapelekea kuzitambua afya zao pamoja na kuanza matibabu maramoja
pale watakapogundulika na magonjwa mbalimbali.
0 Comments