TANGAZA NASI

header ads

NAIBU WAZIRI WA ARDHI AWAKALIA KOONI WADAIWA SUGU WA ARDHI, NJOMBE

 





Na Amiri Kilagalila,Njombe


Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dokta,Angelina Mabula amewaagiza wadaiwa sugu wa madeni ya umiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipa kabla ya kuanza mwaka mpya wa fedha mwezi Juni mwaka huu kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa Mahakamani.


Dokta,Mabula ametoa agizo katika kikao kazi kilichowakutanisha wataalam wa ardhi,wakuu wa wilaya,wabunge na wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa wa Njombe sanjari na ugawaji wa hati za ardhi kwa baadhi ya wakazi wa Njombe ambapo ametaka wadau hao kulipa madeni yao kabla hawajafikishwa mahakamani.


“Wanapendelea kupata hati wasigeuke kuwa wadaiwa sugu,kwasababu leo unapewa hati yako lakini ukiangalia takwimu za ulipaji kodi kwa mwaka,wengi ziko chini ya elfu 10000,zikienda sana 20,000 elfu 30,000 inategemeana na matumizi.Ukiweza kulipa kila mwaka hautakaa uingie kwenye orodha ya wadaiwa sugu”alisema Mabula


Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho akiwemo mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga,mbunge wa ludewa Joseph Kamonga na mkuu wa wilaya ya Makete Veronica Kessy wamemuomba naibu waziri huyo kuwaongezea wataalam wa ardhi katika maeneo yao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanishi mkubwa kwa lengo la kuondoa migogoro ya ardhi.


“Pale Makambako ndio jicho la mkoa wa Njombe sasa mtu anapokaimu anakuwa kama anapimwa hivi,kwa hiyo anakuwa hana maamuzi sahihi”alisema Deo Sanga


“Wananchi wa Ludewa wanamatarajio makubwa,wanahitaji mtaalamu na mbobevu wa sekta ya ardhi kwa hiyo ninaomba mniongezee wataalamu ninaamini tutafanya kazi kubwa sana”alisema mbunge wa Ludewa Joseph Kamonga


Kwa upande wao wananchi na wadaiwa hao wamesema kumekuwa kukiibuka kwa migogoro pindi wanapomilikishwa viwanja hivyo jambo ambalo limekuwa likisababisha kusimama kulipa kodi ya ardhi.


Post a Comment

0 Comments