TANGAZA NASI

header ads

Hofu ya UN juu ya mapigano yanayoendelea Somalia

 


Vikosi vya Usalama vya Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOM), vimeelezea kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya mzozo wa usiku wa manane nchini Somalia.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye akaunti ya Twitter ya UNSOM baada ya mapigano kutokea katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia,  pande zote husika zilitakiwa kuzingatia utulivu.

Taarifa hiyo ya UNSOM ambayo ilihimiza mazungumzo ya kumaliza mvutano, pia ilisema,

"Mizozo hiyo inaonyesha kuwa serikali kuu na serikali za majimbo lazima zikutane pamoja ili kufanya uchaguzi wa tarehe 17 Septemba."

Mvutano huo bado unaendelea baada ya mapigano kutokea Mogadishu.

Vikosi vya usalama vilijibu kwa ghasia ombi la wagombea urais wa upinzani wakiongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Hassan Ali Khaire kutaka kuandamana katika eneo la karibu na uwanja wa ndege asubuhi ya leo.

Katika mapigano kati ya pande hizo mbili, tawi la benki ya Dahabshil la uwanja wa ndege liliteketezwa baada ya shambulizi la kombora.

Wagombea urais wa upinzani wa Somalia walitoa wito kwa umma kuingia mitaani mnamo Februari 15 kumpinga Rais Mohammed Abdullah Farmaju kubakia madarani licha ya muda wake kumalizika tarehe 8 Februari.

Post a Comment

0 Comments