Na Amiri Kilagalila,Njombe
Zaidi ya wananchi 455 wakazi wa kijiji cha Madihani
wilayani Ludewa mkoani Njombe wanatarajia kunufaika moja kwa moja kutokana na
kuanza ujenzi wa mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Rumakali uliopo
katika kijiji hicho.
Treyphon Mbalape ni afisa mtendaji wa kijiji cha
Madihani na Elias Sanga ni mmoja wa wakazi wa kijiji hicho,wamesema kuanza kwa
mradi huo waliousikia tangu mwaka 1998 utafungua fursa kwao na na wilaya ya
Makete kwa kuwa wamekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa nishati.
“Naimani kupitia mradi huu tutanufaika na umeme kwa
kuongeza uzarishaji ndani ya kijiji na ajira zitaongezeka,lakini tunaendelea
kushirikiana kwa ajili ya kutunza vyanzo vya maji ili kulinda mto huu uendelee
kuzalisha maji zaidi”alisema Treyphon Mbalape
Elias Sanga amesema “Kwa kweli tulikuwa tunapata
shaida sana huku vijijina kwa hiyo serikali inapotuletea miradi kama hii
tunaamini tutapona na hali tuliyokuwa nayo”
Mhandisi Toto Zedekia ni meneja wa undelezaji vyanzo
vya umeme akiwa pamoja na timu ya watalamu kutoka shirika la umeme Tanzania
Tanesco pamoja watalamu kutoka wizara ya nishati wamekagua eneo la ujenzi wa
mradi,amesema mradi huo unaotajiwa kuanza karibuni unategemewa kuongeza kiwango
cha umeme nchini kwa kuzalisha megawati (MW) 222.
“Hapa kutakuwa na bwawa ambalo litakuwa na uwezo wa
kubeba kiasi cha meta za ujazo milioni 256,manufaa ya mradi yatakuwa ni makubwa
kwasababu nchi itaingia kwenye uchumi wa viwanda kwa hiyo utachangia kwa kiasi
kikubwa kuongeza umeme kwa ajili ya umeme”alisema Toto Zedekia
Injinia Costa Rubagumya ni Meneja mwandamizi mipango mkakati,amesema
wametembelea eneo la mradi kwa ajili ya maandalizi ya miundombinu ya mwanzo
ikiwemo huduma ya barabara ili kurahisisha utekelezaji wa mradi huku akiomba
wananchi kuendelea kuwa na imani pamoja na kuupokea mradi kwa kuwa vijiji vyote vitakavyopitiwa na mradi watakuwa
ni wanufaika namba moja.
“Serikali inapoleta laini ya umeme kwenye eneo la
utekelezaji wa mradi,vijiji vyote ambavyo vinapitiwa na laini vinakuwa ni vya
kwanza kupatiwa umeme”alisema Injinia Costa Rubagumya
0 Comments