Mwenyekiti Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Jimbo la Magomeni Ussi Jecha Haji amesema vijana wataendelea kutekeleza kwa vitendo Ilani ya chama hicho na maagizo ya serikali ya kufanya usafi maeneo yote ili kuepukana maradhi mbali mbali ya mripuko.
Ameyasema hayo wakati wlipokuwa wakifanya Usafi katika jimbo hilo kwa lengo la kuweka Mazingira safi ndani ya Mji wa Zanzibar.
Amesema zoezi hilo limewapa hamasa kubwa Vijana na kuwa na mwamko wa kushirikiana kwa pamoja kutekeleza agizo hilo kuwa endelevu ili kudumisha usafi nchini.
Mbunge wa Jimbo hilo Mwanakhamisi Kassim alisema Vijana wamehamasika sana kuunga mkono maagizo ya serikali ya kufanya usafi maeneo yote nchini ili kuimarisha uchumi na zaidi kuwapa kipaumbele vijana katika kuleta maendeleo.
Bi Mwanakhamis alieleza kuwa watashirikiana vizuri na vijana na kuwalea katika malezi mazuri yatakayoleta maendeleo ili kufikia uchumi wa Buluu ili kupata taifa imara.
Nae Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Magomeni ambae pia ni Mlezi wa Jumuiya za Chama hicho Mwanaidi Abdallah Sleiman alisema zoezi la kufanya usafi litakuwa endelevu ili kuweka mazingira na yenye kuvutia.
Nao vijana hao waliwashukuru viongozi wao kwa kuwapa ushirikiano na kuwa pamoja katika zoezi hilo na kuwataka Vijana wengine kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao wasisubiri agizo kwani usafi ni jukumu la wote.
Usafi huo waliofanya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Magomeni utakuwa ni muendelezo kwa kila wiki ili kuweka Mji safi.
0 Comments