TANGAZA NASI

header ads

Uongozi wa KMC FC wamsimamisha mchezaji Realint Lusajo sababu ya utovu wa nidhamu

 



Uongozi wa Timu ya KMC FC unapenda kuwajulisha mashabiki na wapenzi wa Timu ya KMC FC kuwa mchezaji Realint Lusajo amesimamishwa kutokana na sababu ya utovu wa nidhamu.

Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni baada ya uongozi kujiridhisha na kwamba mchezaji yoyote anapofanya makosa ya utovu wa nidhamu kwenye Timu atapaswa kupata adhabu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa.

Wakati huo huo,uongozi wa KMC FC pia umetoa mapumziko ya siku 10 kwa wachezaji wake na kwamba watapaswa kurejea kambini Januari 15 mwaka huu kwa ajili ya kuanza maandalizi ya michezo ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara ambapo mchezo unaofuata KMC FC watakuwa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons.

Post a Comment

0 Comments