BAADA ya kikosi cha Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya Makundi Afrika, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara awashukuru mashabiki.
Kupitia Ukurasa wake rasmi wa Istagram anaandika namna hii:" Nahisi mimi ni miongoni mwa watu wenye bahati kubwa kufanya kazi na kizazi cha wachezaji hawa.
"Fikiria kwa ubongo jinsi ambavyo ningeraruliwa huku mitandaoni iwapo Simba ingetolewa jana.
Najiuliza matusi mangapi yalikuwa yananisubiri ?
"War in Dar,(WIDA) ingegeuzwa geuzwa na kashfa za aina ngapi? Sasa hivi kungekuwa na picha zangu ngapi za kunidhihaki mitandaoni?
"Mungu wangu Rahmani nitaendelea kukushukuru kwa karama zako kwangu na umenipa deni kubwa kwa wachezaji hawa nnaowapenda sana.Wamenistiri mimi na Wanasimba wote.
"Ila na mimi nimo,ndio msemaji pekee kutoka Afrika Mashariki ambae klabu yake itacheza fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.
"Najionea fahari kubwa kuwa sehemu ya Simba, asanteni asanteni Watanzania wote,"
0 Comments