TANGAZA NASI

header ads

Serikali kuanza ujenzi wa mradi wa umeme mto Ruhuji utakaozalisha zaidi ya Megawati 358 Njombe

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Zaidi ya Megawati 358 za umeme zinatarajia kuzalishwa baada ya kukamilika kwa mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya mto Ruhuji uliopo halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo unaotarajia kuanza mwezi June 2021.

Amebanisha hayo naibu katibu mkuu wa nishati mhandisi Leonard Masanja,alipoongozana na timu ya wataalamu kutoka wizara ya nishati pamoja na Tanesco walipofika na kukagua eneo la ujenzi wa mradi uliopo kijiji cha Itipula mjini Njombe.

“Serikali imeelekeza tuanze utekelezaji wa ujenzi wa mradi na kufuatia maelekezo hayo timu ya wataalamu imeshaudwa,na tumeshapata watalamu takribani 10 ambao wataongozwa na wizara ya nishati”alisema Leonard Masanja

Amesema usanifu wa mwanzo ulifanyika mwaka 1998 na kubaini eneo hilo linaloitwa Zanzibery panafaa kujegwa bwawa la kukinga maji na kwa kuzingatia uharaka wa mradi pamoja na mahitaji ya umeme kwenye uchumi wa viwanda wameanza maandalizi stahiki.

“Mradi huu ni kati ya miradi muhimu ambayo imetarajiwa siku nyigi kujegwa lakini kwa sababu mbali mbali tulikuwa hatujafikia hatua a kunza kujenga na sasa hivi ni kipindi cha kazi na mradi huu utajengwa”aliongeza Masanja

Dkt,Tito Mwinuka ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme Tanzania Tanesco.Amesema wamejpanga kuuteeleza mradi huo wa kadri ya maelekezo kwa kuwa kukamlia wa mradi kutasadia kuongeza kiasi cha umeme kwenye gridi ya taifa.

“Megawati 358 zitaweza kupatikana hapa kwa hiyo maana yake utaweza kusaidia wanachi kumudu ghalama za umeme”alisema Mwinuka

Josphat Mwenda ni mwenyekiti wa kijiji cha Itipula na Eleteus Mkolwa ni mwanachi wa kijiji hicho,wamesema kuanzishwa kwa mradi huo mkubwa wanaamini watanufaika kwa kiasi kikubwa.

“Vijana watanufaika na mradi kwa kufanya kazi kutokana na ajira za mda lakini pia hata umeme ukishafika tunaamini kazi zinazohitaji umeme zitafanyika kirahisi”alisema Mkolwa.

Mradi huo uliosubiriwa kwa zaidi ya miaka 22 unatarajiwa kujengwa mabwawa mawili inteki moja pamoja na miudombinu mingine kwa miezi 36 .

Post a Comment

0 Comments