Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Hamad kwa maaamuzi yake aliyoyafanya yakuungana na serikali ya umoja wa kitaifa.
Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kushoto ni Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Hamad wakipeana mikono na katika ni Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi.
Magufuli ametoa pongezi hizo katika ziara ya Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi aakiongozana na makamu huyo wa kwanza Rais mkoani Geita wilaya ya Chato ambapo amesema Maalim Seif ni kiongozi kweli na amefanya maamuzi ya kishujaa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Hamad alipowasili Ikulu ndogo ya Chato, Katikati ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
“Nakupongeza Maalim Seif kwanza kwa kukubali kuwa miongoni mwa serikali inayoongozwa na Hussein Mwinyi, kuwa miongoni mwa serikali ya umoja wa kitaifa, Maalim Seif amefanya kazi na mzee Mwinyi na leo amekuja kufanya kazi na mtoto ujuzi wa Maalim Seif katika uongozi ni mkubwa, ujuzi wake na uongozi wake tunaihitaji katika uongozi wa sasa na ndio maana nilimpongeza sana kwa maamuzi yake yale ni maamuzi ya kishujaa na yanamueleko na muongozo wa Mwenyezi Mungu” amesema Rais Magufuli
Aidha Rais Magufuli amempongeza Maalim kwa kutozingatia maslahi yake badala yake kujitoa muhanga kwa ajili ya maslahai ya Wazanzibari wote huku akiahidi kutoa msaada wake hali na mali kwa viongozi hao wawili kwa uongozi wao ambao umeanza kuleta mwanga kwa Zanzibar.
Leo Dkt.Mwinyi amefanya ziara Chato akiongozana na Makamu wake wa kwanza Maalim Seif Sharrif Hamad ambapo wamekuwa na majadiliano na Rais Magufuli ambaye amewaahidi kuwa nao bega kwa bega huku akiwapongeza kwa kuadhimisha sherehe za mapinduzi ya Zanzibar.
0 Comments