TANGAZA NASI

header ads

Naibu waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI aridhishwa na ujenzi wa shule Bora ya mfano Nchini.

 


Na Woinde Shizza ,ARUSHA

  waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI David Sindile  ameridhishwa na ujenzi wa shule  ya Sekondari ya Mfano nchini ya Patandi maalum iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Wilayani Arumeru.

Haya yamejiri wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotelelezwa kwa Mpango wa Lipa kutokana na Matokeo (EP4R) katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru  ambapo amepongeza ujenzi wa shule ya Sekondari ya Patandi maalum iliyogharimu zaidi ya Bilioni 3.

 Silinde  ameeleza kuwa Serikali mbali na kutoa fedha za ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia mpango wa EP4R  imeweka mikakati ya kuendelea   kuboresha  sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya kufundishia  na kujifunzia kwa kuanza ujenzi wa shule za Sekondari 1000 .

Aidha, Silinde amesema ujenzi wa shule hizo 1000  utafanyika  kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza shule 154 zitajengwa.

 Silinde amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro kwa usimamizi wa miradi Wilayani humo sambamba na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Meru  na Arusha kwa ubunifu na utendaji kazi wenye tija katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa na utekelezaji wa Miradi ya P4R .

Naye Dkt.John D. Pallangyo,  Mbunge wa Jimbo la Arumeru la Mashariki ameishukuru Serikali kwa kuongeza thamani ya Jimbo la Arumeru Mashariki kwa ujenzi wa shule hiyo.

Aidha, katika utatuzi wa changamoto za upatikanaji wa maji, kuongeza miundombinu ya taka, Nyumba za Walimu na Genereta zilizowasilishwa na Mwl.Janeth Mollel ambaye ni  Mkuu wa shule ya Sekondari ya Patandi Maalum, Silinde  ameeleza kuwa Serikali imelipokea na itatoa fedha mapema .

Katika ziara hiyo Waziri alikagua pia ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa katika shule ya Sekondari Sing’isi vilivyojengwa kupitia Programu ya EP4R

Post a Comment

0 Comments