Mgombea wa urais nchini Uganda, Bobi Wine amepinga matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa hadi sasa na kujitaja binafsi kama rais mteuli, licha ya tume ya uchaguzi kusema kuwa sio kura zote zilizokwisha hesabiwa.
Bobi Wine anadai uchaguzi wa Alhamisi ulitawaliwa na wizi mbaya zaidi wa kura kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Uganda, lakini hakutoa ushahidi wowote kuhusu madai yake.
Ametangaza kuwa mapambano ndio kwanza yameanza.
Bobi Wine, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi, anasema kuwa atazungumza na waandishi wa habari tena mnamo saa chache zijazo juu ya kitakachofuatia.
Matokeo ya awali yanayotolewa na Tume ya uchaguzi yanaonesha Rais Yoweri Museveni anaongoza kwa zaidi ya 60%.
Wakati huohuo wanajeshi wakiwa wamezingira nyumba ya Bobi Wine.
0 Comments