TANGAZA NASI

header ads

Mshirika mkuu wa Trump Mitch McConnell avunja kimya na kumpongeza Biden



 Afisa wa ngazi ya juu wa chama cha Republican cha Donald Trump, ambaye ndiye kiongozi wa wengi katika bunge la Seneti La Marekani-Mitch McConnell, amempongeza Joe Biden kwa ushindi wake katika uchaguzi wa urais mwezi uliopita.

Senata McConnell alizungumza baada ya wajumbe wa uchaguzi -electoral college kuidhinisha rasmi ushindi wa Bw Biden dhidi ya Trump.

Mdemocrat alishinda kura za wajumbe 306 dhidi ya Trump ambaye alipata kura 232.

Rais Trump bado amekataa kukubali kushindwa , huku akiendelea kutoa madai yasiyo na ushahidi ya wizi mkubwa wa kura.

Mahusiano ya na bunge la Seneti ambalo kwa sasa linadhibitiwa na Warepublican c, yatakuwa muhimu kwa urais wa Bw Biden.

Rais wa Marekani hachaguliwi mara moja na wapigakura,bali kile kinachoitwa electoral college

Post a Comment

0 Comments