TANGAZA NASI

header ads

Madaktari waanza mgomo Kenya

 


Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali za serikali nchini Kenya, wameanza mgomo wa kote nchini, wakilalamikia kutopewa bima ya afya, na ukosefu wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona wanapowashughulikia wagonjwa walioambukizwa virusi hivyo.

Mgomo huo umeanza jana baada ya muungano wa madaktari, wanafamasia na madaktari wa meno kusema kwamba serikali imekosa kushughulika mahitaji yao kwa mda wa miezi nane iliyopita.

Muungano huo umesema kwamba serikali ya Kenya imepuuza maslahi ya wafanyakazi wa afya nchini humo.

Kulingana na muungano huo, madkatari 14 wamekufa kutokana na virusi vya Corona nchini Kenya, tangu kisa cha kwanza kiliporipotiwa mwezi Machi mwaka huu.

Mgomo huo ulikuwa umepangiwa kuanza Desemba 7, lakini ukaahirishwa kwa mda wa wiki mbili ili kuruhusu mazungumzo kati ya viongozi wa madaktari na serikali, kufanyika.

Post a Comment

0 Comments