TANGAZA NASI

header ads

Jamii wilayani Makete yapewa elimu namna ya kuimarisha ndoa zao

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kufuata misingi ya ndoa ili kuimarisha ndoa zao na kuepusha migogoro ya familia inayosabisha kuvunjika kwa ndoa nyingi wilayani humo na watoto kukosa malezi bora.

Wito ulitolewa juzi na baadhi ya wachungaji kutoka madhehebu mbali mbali katika kongamano la ndoa lililofanyika katika halmashauri hiyo kwa lengo la kupunguza ukatili kwenye ndoa na kujenga kizazi imara nadani ya jamii ya wilaya ya Makete.



Alex Nkwama ni mchungaji wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa tumaini,lisema licha ya ndoa nyingi kuvunjika kutokana ni migogoro lakini sababu kubwa ni kutokana na wengi kuingia kwenye ndoa kinyume na wakati sahihi.Huku Leah Sowo mama mchungaji kutoka kanisa la bonde la Baraka akiwataka wanandoa kuelewana kuanzia sifa mpaka tabia ili kuendelea kutunza ndoa zao kwa kuwa ndoa ni mchakato wa muda mrefu.

“Wengi mpaka leo wameingia kwenye ndoa,uvhumba na mahusiano kinyume na wakati sahihi na Biblia kitabu cha Mwanzo 2:18 inaeleza vizuri kabisa.sasa wengi wameenda kinyume na wakati sahihi ndio maana wanaumizwa,wanajuta na kulia kwenye ndoa zao”alisema mchungaji Alex Nkwama.



Emma Mzunda na Yese Kyando ni miongoni mwa wa shiriki katika kongamano hilo walisema yapo mambo makubwa waliojifunza kwa kuwa zipo changamoto nyingi katika ndoa zinazopelekea kuharibika kwa ndoa ikiwemo kukaa kimya yanapotokea matatizo huku wakitoa wito kwa jamii kuendelea kuwa wazi kwa watu wanao waamini ili kupata msaada katika ndoa zao.    


 

Kwa upande wake Lulu Samson mratibu wa kongamano hilo linaloandaliwa na umoja wa tumaini kwa Bwana,alisema kongamano hilo limeanziswa kwa malengo makuu matatu mara baada ya kuona ndoa nyingi zinavunjika na kusababisha malezi yasiyo bora kwa watoto.

“Lakini pia kuna swala jingine la ukatili wa pande zote mbili kwenye ndoa ndio maana tukaanzisha kongamano hili  ili kuweka usawa na ushirikiano kwenye ndoa”alisema Lulu Samson



Rabson Mahenge ni daktari wa binadamu kitaaluma na mtaalamu wa mahusiano,alitoa wito kwa wanandoa kuwa wasafi ili kuboresha mahusiaono yao huku akiomba waandaaji wa kongamano hilo kuongeza nguvu ili kuponya ndoa nyingi kwenye jamaa.

“Nimepend a kitu kikubwa hapa lakini bado watu hawajakipa thamani nah ii ni sehemu ambayo watu inabidi wapone na wabadirike,nafikiri watu waone haya makongamano ni muhimu wapone na baadaye tuandae hata safari za ndoa watu wapone zaidi sio kila siku kukaa sehemu moja”alisema Rbson Mahenge

Post a Comment

0 Comments