Na Amiri Kilagalila,Njombe
Kutokana na Hasara
Kubwa Inayopatikana Kwa Mkulima wakati wa Kupukucha mahindi aliyolima kwa
Gharama Kubwa Kwa Kukosa Nyenzo za Kisasa Wadau wa Kilimo Nchini Wamelazimika kukabidhi
Nyenzo (mashine) za Kupukucha mazao Kupitia Mradi wa TAPBDs Chini ya Ufadhili
wa AGRA.
Kwa Kuliona Hilo
Shirika la TAPBDS Limelazimika Kutafuta Fedha Zaidi ya Shilingi Milioni 60
Chini ya Ufadhili wa Shirika la AGRA na Kununua Zana za Kisasa Yakiwemo
Maguta,Pikipiki na Mashine za Kupukucha Mahindi na Kuwapa Wakulima na
Wajasiriamali Wasindikaji wa Nafaka Ili Waweze Kupata Mahindi Yenye Ubora
Katika Masoko ya Ndani na Kimataifa Ambapo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TAPDS Deodati
Bernard na Theresia Kato Ambaye ni Mshauri wa Biashara wa TAPBDS Wanasema Hii
Itakuwa Msaada Mkubwa kwa Mkulima Katika Kupunguza Upotevu wa Mazao.
“Kupitia mradi wa PATA
TIJA ambao pia unasimamiwa na AGRA tumeweza kuwafikia wakulima zaidi ya elfu thelathini
kuanzia mwaka 2017 tulivyoanza mradi .Tumeweza pia kuwafikia na kutoa huduma
mbali mbali kwa wajasiriamali zaidi ya 250 katika ukanda huu wa kusini ikiwemo
pia biashara za vijana 30 waliowezeshwa zaidi ya milioni 60”alisema Deodati
Bernard Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TAPDS
“Vitu ambavyo
vimetolewa ni mashine ya kupukuchua,pikipiki kwasababu mashine ya kupukuchua
inahitajika kwenda shamba moja kwenda jingine.lakini pia piki piki ya miguu
mitatu kwasababu kuna mshine nyingine ni nzito haiwezi kubebwa na piki piki
“alisema Theresia Kato Mshauri wa Biashara wa TAPBDS
Mgeni wa Heshima wakati
wa kukabidhi Mashine Hizo ni Katibu Tawala Sehemu za Uchumi na Uzalishaji Mkoa
wa Njombe Bwana Ayoub Mndeme Kwa Niaba ya Katibu Tawala Mkoa Anasema Anatarajia
Kuona Teknolojia Hiyo Inatolewa Kwa Wakulima na Wajasiriamali Wengi Zaidi
Kusini Mwa Tanzania Kauli Inayoungwa Mkono na Maofisa Kilimo wa Mikoa ya
Njombe,Iringa na Ruvuma.
“Pamoja na ugeni wa
teknolojia hii nina imani kwamba maafisa wa serikali waliojumuika katika hafla
hii,watasaidia kuendelea kuelimisha wakulima kuhusu umuhimu wa matumizi yake
ili kuleta tija kwa mazao yanayotoka Tanzania hasa kwa mkoa wa Njombe na mikoa
mingine jirani “alisema Ayoub Mndeme Kwa Niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Njombe
“Ili mashine hizi
ziafanye kazi kwa kiwango kinachostahili lazima kuwe kuna mahindi ya kutosha
kwa hiyo kwa kushirikiana na wadau tunaenda kuhakikisha angalau uzalishaji
unaongezeka”alisema afisa kilimo wa mkoa wa Iringa
“Tunaendelea kuwaomba
wadau wetu katika mambo mengine kama itawezekana kwasababu naona wameanza kule
mwisho kwenye kupukuchua lakini kuna kupanda halafu kupalilia na kadhalika kwa hiyo kama wanaweza pia
kutusaidia mashine ndogo ndogo ili hii chaeni nzima tuwe nazo”alisema afisa
kilimo wa mkoa wa Ruvuma
Lucy Kitavile Maarufu
Kama Mama Seki na Ibrahim Mhesi Kwa Niaba ya Wakulima Waliopatiwa Zana Hizo
Kama Ruzuku Wanasema Sasa Watakwenda Kupata Nafaka Zenye Ubora wa Hali ya Juu
Zitakazokubalika Katika Masoko ya Ndani na Nje.
“Kwa kweli awali nilikuwa
nafanya kazi kwa mazingira magumu mmno nilikuwa napiga mahindi kwa kutumia miti
lakini kuanzia leo niko vizuri na
ninaamini itanisaidia katika shughuli zangu lakini pia na wengine”alisema Lucy
Kitavile Maarufu Kama Mama Seki mkulima wa Njombe
Mradi huo wenye lengo
la kupunguza upotezu wa mazao shambani upo katika mikoa ya
Njombe,Ruvuma,Iringa,Kagera,Kigoma,Katavi na Mbeya umeanza kwa hatua mbali
mbali za kuwapata wakulima/wafanyabiashara kwa kuomba ruzuku huku kwa kanda ya
kusini wakipokea vifaa hivyo wakulima 17 waliofanikiwa kukidhi vigezo.
0 Comments