Na Amiri Kilagalila,Njombe
Shekhe mkuu wa wilaya ya Njombe Mikidadi Shabani Dinga, amewapongeza waumini wa dini ya kiislamu kufanikisha uchaguzi mkuu wa Rais,Ubunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu kumalizika kwa amani na utulivu na kuyaishi maandiko matakatifu yaliyoandikwa katika kitabu cha Quran Tukufu.
ametoa shukrani wakati akitoa salamu kwa waumini wa dini ya kiislamu wakati wakisheherekea Maulid ya siku ya kuzaliwa Mtume Mohamed iliyowashirikisha pia waumini wa wadini hiyo kutoka mikoa ya Iringa na Mbeya..
"Waislamu nikupongezeni kwa utulivu mkubwa mliouonyesha wakati wa uchaguzi ,kwa nidhamu kubwa mlioonyesha kwa serikali yetu na nina imani mliishi katika maisha aliyotufundisha mtume wetu Mohamed,mmetulia kipindi cha kampeni na mkatulia vizuri kipindi cha uchaguzi"alisema Mikidadi Shabani Dinga
Sherehe ya Maulid huadhimishwa na waumini wa kiislam kwa kwenda sambamba na kusoma Quran Tukufu, kusikiliza mawaidha pamoja na nyimbo za Kaswida ambao baadhi ya mawaidha yaliyotolewa..
Baadhi ya waumini wa kiislamu walioshiriki sherehe hiyo wamesema
"Lengo la kukutana kwetu ni kukumbushana yale ambayo mtume Mohamed ametuamrisha na yale ambayo mwenyezi Mungu ameyakataza na pia kuimarisha amani mshikamano na undugu"alisema Hawati Nasibu
Hatua ya pongezi imekuja mara baada ya kufanyika uchaguzi kwa amani kufuatia kuwepo na hofu iliyotokana na baadhi ya viongozi wa dini kuonyesha kuegemea upande wakati wa kampeni.
0 Comments