TANGAZA NASI

header ads

Mamia ya wananchi wa Pakistan waandamana kumpinga Macron

 


Wananchi wa Pakistan wamefanya maandamano ya kumpinga Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa matamshi yake dhidi ya Uislamu na Nabii Muhammed. 

Mamia ya wananchi wa chama cha Tahrik-i Lebbeyk Pakistan (TLP) walikusanyika pamoja kwenye eneo la Chadni Chowk lililoko mjini Rawalpindi, na kutembea huku kuelekea ubalozi wa Ufaransa ulioko katika mji mkuu wa Islamabad huku wakitoa kaulimbiu dhidi ya Macron.

Vikosi vya usalama viliweka vizuizi vya makontena zaidi ya 300 kwenye barabara za kuingia na kutoka mji mkuu wa Islamabad ili kudhibiti hali ya usalama. 

Kwa upande mwingine, vurugu zilitokea kati ya waandamanaji na maafisa wa polisi waliokuwa wakijaribu kuwazuia kuingia mji mkuu.

Maafisa wa polisi walitumia mabomu ya machozi ili kukabiliana na kuwatawanya waandamanaji. 

Barabara za maeneo muhimu yenye majengo ya serikali kama vile ofisi za bunge, wizara na balozi pia zilifungwa kwa makontena.

Hapo awali, maandamano ya kumpinga Rais wa Ufaransa Macron pia yaliwahi kufanyika katika miji mbalimbali ya Pakistan kama vile Karachi, Lahore, Pashawar na Islamabad. 

Post a Comment

0 Comments