TANGAZA NASI

header ads

EAGT kanda ya nyanda za juu kusini Mashariki yapata viongozi wapya



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Ikiwa ni Utaratibu wa Kanisa la EAGT Kila Baada ya Miaka Mitano kupata viongozi watakao waongoza kwa kuwapigia kura hatimaye EAGT Kanda ya nyanda za juu kusini  mashariki wameweza kuchagua na kuwapata askofu wa kanda, makamu askofu katibu na muweka hazina watakao shika nafasi hizo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Uchaguzi huo ulio hudhuriwa na wachungaji takribani 417 wa kanda hiyo katika kanisa la EAGT lililopo Njombe mjini wakiongozwa na askofu mkuu wa EAGT Tanzania Dkt,Brown Mwakipesile,wamefanikisha zoezi la kuwachagua viongozi hoa wa kiroho kama ambavyo utaratibu wa kanisa hilo unavyo elekeza namna ya kupata viongozi wao.

Katika zoezi la uchaguzi huo amabo hufanyika kila baada ya miaka mitano Hatimaye Askofu Rafael kayombo ameweza kutetea kiti chake cha uaskofu kwa kupata kura 241 licha ya kuto fikia Theluthi tatu ya wapiga kura 417 ambayo ni kura 278 Lakini kwa kufuata utaratibu sahihi wa upigaji kura ameibuka mshindi na kumuacha makamu wake kwa kura nyingi.

Aidha Katika Nafasi ya Makamu askofu wa kanisa hilo kanda ya ya nyanda za juu kusini Mashariki ,wachungaji na wainjilisti wamempa ridhaa Alfredi Mwagike kwa Kupata kura 331 huku naye akitetea kiti chake  ambapo alipata kura nyingi na kuvuka theluthitatu ya wapiga kura 417 na kutangazwa kuwa makamu askofu kanda ya nyanda za juu kusini mashariki kwa miaka mitano mingine.


Katika uchaguzi huo katibu wa kanisa alipaswa kupigiwa kura kutokana na umuhimu wa mhimili wa kanisa hilo hivyo Michael Kilasi alipata ushindi wa kura 346 na kupata ridhaa ya kuwa kiongozi wa kanisa hilo kama katibu wa kanda kwa miaka mitano lakini mara baada ya kupata nafasi ya kuzungmza kiongozi aliwashukuru wachungaji na wainjilisti  kwa kumchagua na kuahidi kwenda kufanya kazi kwa nguvu kiroho na kuhakikisha makanisa yanaenda kujengwa pamoja na kuongeza waamini.

Ili Kufikia lengo la kukamilisha Safu ya Uongozi mweka Hazina wa Kanisa alipatikana kwa ushindi wa kura 375 kati ya kura 417 zilizopigwa  ambapo ndugu Osmundi Mlowe anakuwa mweka hazina wa kanisa la EAGT Kwa Miaka Mingine Mitano hivyo amewasihi waamini wa kanisa kuweka masilahi ya kanisa mbele ili kufikia malengo waliyo nayo kwa sasa.

Uchaguzi wa kuwapata viongozi wa kiroho katika kanisa la EAGT kanda ya nyanda za juu kusini mashariki umesimamiwa na askofu Mkuu wa EAGT Tanzania akishirikiana na safu ya uongoziwake kutoka makao makuu  hivyo amewataka viongozi walio chaguliwa kwenda kueneza Imani kwa waamini na kulijenga kanisa kwani EAGT Limekuwa ndio kanisa lenye misingi thabiti wa kuigwa na makanisa mengine Nchini.

Post a Comment

0 Comments