Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Ili kuinua uchumi wa
familia na jamii kanisa la KKKT makao makuu limetoa msaada wa fedha shilingi
million 63 kwa wananchi katika wilaya za wangingombe na makete mkoani
Njombe kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali na kilimo cha
parachichi.
Akikabidhi hundi kwa
maaskofu wa dayosisi za Kusini kati Njombe na dayosisi ya kusini mgharibi
askofu mkuu wa kanisala KKKT Dkt ,Fredrick
Shoo amesema msaada huo unalenga kuwainua wanufaika kiuchumi hasa wanawake .
“Kipato kinapoongezeka
basi hata hali ya maisha inakuwa naafuu kwa kumudu matibabu,elimu na hata kuwa
na chakula cha kutosha ,niombe wahusika na walengwa waweze kutumia mradi huu
vizuri” Dkt ,Fredrick Shoo Askofu mkuu wa KKKT
“Kanisa linahubiri
Injiri kwa maneno na matendo wakati wachungaji wetu wanahubiri Injili
madhabahuni na mradi huu unapita kuhubiri kwa njia ya vitendo kwa kuimarisha na
kuboresha uchumi na katika mradi huu maeneo mengine kanisa linatoa mradi wa Ng’ombe
bora wa maziwa”alisema Patricia Mwaikenda mratibu wa mpango wa maisha endelevu
kanisa la KKKT
Maskofu kutoka
dayosisi zenye wanufaika wa msaada huo wameeleza namna utakavyo kuwa chachu ya
maendeleo
“Ni hatua kubwa sana
kwa kanisa kutembea na watu wake kiuchumi na sio kiroho tu na msaada huu
utawatoa kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine katika kujikimu na kuleta
maendeleo ya maisha yao” Dkt,Marc George Fihavango askofu wa dayosisi ya
kusini
“Hela mlizotupa tunashukuru sana na tunaamini
tutafanikiwa ili pia na wenzetu ambao bado hawajapata waweze kunufaika”alisema Luhwishye
Chengula mnufaika kutoka Ikuwo Makete
Wanufaika na msaada
huo unaotolewa na kanisa ni Pamoja na wanawakewajasiria mali waliko
katika vikundi na wakulima wa matunda aina ya parachichi.
0 Comments