TANGAZA NASI

header ads

Aliyetoroka gerezani auawa na polisi Njombe

 



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Izack Kawogo mkazi wa Njombe,ameuawa na jeshi la  Polisi mjini Njombe usiku wa kuamkia Novemba 20  baada ya kumjeruhi kaka yake Andreas Kawogo (61) kwa kumpiga risasi mbili begani kwa kutumia siraha aina ya SMG Uzgun, huku pia akituhumiwa kujihusisha na masuala ya unyang'anyi na ujambazi.

Kamanda wa jeshi la polisi Hamisi Issa amesema marehemu alikuwa na matukio ya unyang'anyi kipindi cha nyuma jambo ambalo lilipelekea kufungwa jera miaka 30 na kisha kuhamishiwa gereza la Iringa ambako alimjeruhi askari magereza kwa panga na kisha kutoroka na siraha hiyo ikiwa na risasi kumi.

Kamanda Issa amesema vikosi vya ulinzi na usalama vimemshambulia kwa risasi mtuhumiwa huyo ambaye tayari ni marehemu baada ya kumpiga risasi kaka yake kwa madai ya kwamba ameuza mali zake na kushindwa kumtoa gerezani wakati akitumikia kifungo.

“Usiku wa leo kuna mtu ameuawa kwa kupigwa risasi na askari baada ya mtu huyu kumjeruhi kaka yake.Na kuna matukio alifanya huko Iringa alimshambulia askari magereza kwa kapanga na matokeo yake akasababisha wafungwa wengine wakatoroka nay eye alichukua siraha aina ya Uzgun”Alisema Kamanda Issa

 

“Hii ni siraha ambayo askari magereza wanaitumia kwa ajili ya ulinzi wa wafungwa hao kwa hiyo tangu atoroke na hiyo siraha akawa anaitumia kwenye uhalifu kwa hiyo huyu ni muarifu sugu bahati mbaya ametutoka na sasa hivi amebadili maisha amenda Mbinguni”aliongeza tena

Aidha Kamanda amesema wakati uchunguzi unafanyika ili kumnasa mtuhumiwa ndugu walikuwa wazito kutoa ushirikiano licha ya kujua maovu yake jambo ambalo limesababisha kuchelewa kumdhibiti na kisha kutoa rai kwa wananchi na watu wenye tabia za wizi na ujambazi.

“Wananchi wa Njombe wasiwe watu wa kuficha mambo huyu mwenye siraha hii tungeweza kumkamata toka mchana lakini wana ndugu wenyewe pamoja na kuwapa pole lakini walikataa kutuonyesha ,lakini ya kufuatilia hili jambo limefanyika kati ya majeshi yote “aliongeza kamanda Issa

Kuhusu hatua zinazochukuliwa kwa siraha iliyopatikana baada ya kuibiwa gerezani Issa amesema wanakwenda kufanya utaratibu wa kuirudisha katika gereza ilipoibiwa

“Juhudi za kufuatilia hili jambo limefanyika kati ya majeshi yote polisi na magereza na bahati nzuri leo kwasababu Magereza wamekuja na silaha ndio hii hatuna ubishi kuwa ni ya kwao,tutafanya taratibu zote na tutawakabidhi”alimaliza kusema kamanda Issa

Post a Comment

0 Comments