TANGAZA NASI

header ads

Ujerumani yawasilisha bajeti ya euro bilioni 96 kupambana na athari za COVID-19



 Serikali ya Ujerumani imewasilisha bajeti ya dharura ya kukabiliana na athari za kiuchumi za janga la corona itakayoanza kutumika mwakani. 

Akifafanuwa bajeti hiyo inayohitaji mkopo wa euro bilioni 96.2 na iliyotangazwa na Waziri wa Fedha Olaf Schloz, Kansela Angela Merkel aliliambia bunge hapo jana kwamba hiyo ni hatua ya haraka na ya maana kuiwezesha Ujerumani kurejea kwenye maisha ya kawaida haraka iwezekanavyo. 

Ikiwa utapitishwa na Bunge, mkopo wa bajeti hiyo utakuwa ni wa pili kwa ukubwa kwenye historia ya Ujerumani. 

Uwezo wa kukopa kiwango kikubwa kama hicho cha fedha umekuja baada ya serikali kuondoka ukomo wa madeni, ambao kawaida unaizuwia serikali kuu kukopa zaidi ya asilimia 0.35 ya pato jumla la ndani. 

Fedha hizo zitatumika kwenye kuunganisha hatua za kuzisaidia kampuni na biashara zilizoumizwa vibaya na janga la COVID-19. 

Merkel alionya kwamba watu wanapaswa kuendelea kuchukuwa hadhari dhidi ya maambukizo mapya, ili kuepuka kufungwa tena kwa shughuli za kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments