Na Emmanuel Mkulu, Njombe
Wanawake wamepaswa kuwa mfano wa kuigwa wanapo pewa fursa ya elimu ya Ujasilia mali ili wajikwamue kiuchumi na kuwasaidia wengine ambao wanachangamoto ya kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamebainishwa na Maria Mbuya mama mjasilia mali kutoka mkoa wa Mbeya akiwa katika maonesho ya siku ya Chakula na Lishe ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Njombe,na ni mama mjasilia mali mdogo ambaye aliwahi shiriki shindano la mama shujaa na kuibuka mshindi Tanzania mwaka 2016 kutokana na kazi za ujasiliamali alizo kuwa kizifanya.
Aidha Bi.Maria Mbuya anasema amefanikiwa kufika katika maonesho ya siku ya Chakula mkoani Njombe Kupitia shirika la oxfarm ,shirika linalo shughulika na kuibua changamoto za kilimo cha mazao mbalimbali na kuwainua wajasilia mali wadogo hususani wanawake .
“Nimeweza kufika hapa na kufanya haya yote kutokana na shirika la Oxfarm ambalo limejiwekeza kwa ajili ya kuweza kusaidia akina mama wajasilia mali wadogo na kuweza kuwakusanya akina mama nchi nzima bara na visiwani kupitia shindano la mama shujaa wa chakula kwa miaka tofauti tangu mwaka 2012”
Santina mapile ni miongoni mwa mama shujaa kupitia shirika la Oxfarm mwaka 2014 kutoka mkoa wa Njombe anasema mara baada ya ushindi wake mwaka 2014 amefanikiwa pakubwa kwani mpaka sasa anamiliki ekari kumi za parachichi ,zao makakati kwa mkoa wa Njombe ambalo limekuwa likimuingizia kipato cha zaidi ya shilingi milioni moja kwa mwaka na kufanikiwa kutoa ajira kwa akina mama wengine ambao hawajiwezi kiuchumi.
Aidha mratibu kampeni kutoka Oxfam Mkamiti Mgawe amesema maonesho hayo yamekuwa na mafanikio makubwa kwani elimu waliyoitoa itasaidia kubadili mwenendo wa maisha kwa kufuata mfumo mzuri wa ufanyaji kazi."Sisi kama Oxfam tunahakikisha kuwa kuna uwepo wa chakula na kuwasaidia wakulima wadogo wadogo ambao ndiyo wazalishaji wakubwa wa chakula ambao wengi wetu ndiyo tunakula na jamii kwaa ujumla tunatumia" Amsema Mkamiti.
Mkamiti Mgawe ameongeza kuwa shirika la Oxfarm limejikita zaidi katika kutoa elimu ya namana ya utunzaji bora wachakula ili kisipotee na kwamba kama shirika linafanya kazi ya kuwakutanisha wadau mbalimbali wa uuzaji wa pembejeo ,wanunuzi wa mazao pamoja na kufikisha changamoto za wadau hao katika serikali ili ziweze kupatiwa ufumbusi kwa urahisi.
“Tunafikisha Changamoto za wajasilimali wadogo zinazo wakabili katika serikali ,tunawakutanisha na serikali pia watu wanao shughulika na uuzaji wa pembejeo nwanashughulika na ununuaji wa mazao ya chakula lakini pia kuwafikisha Kwa Serikali kuzungumzia changamoto zao wanazo kabiliana nazo pia waweze kurekebisha sera mbalimbali,waweze kuwatafutua masoko amabayo ni rahisi wajasiliamali kufika lakini pia wawezerahisishia mfumo mzima wa kilimo”.
0 Comments