Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Waumini wa kanisa la Kiinjili
la Kiluthel usharika wa Mjimwema mjini Makambako mkoani Njombe wamepigwa
marufuku kuingia ibadani na Nguo,vilemba na kofia zenye nembo au rangi za vyama vya siasa.
Onyo limetolewa na Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Lyosi Mwalyosi,wakati
akizungumza na kituo hiki huku akiwa na lengo la waumini kuheshimu sehemu za
ibada kwa kuepusha itikadi za vyama.
Vile vile mchungaji
huyo amewataka wanasiasa na waumini wote wanaoabudu katika kanisa hilo kuacha
tabia ya kuitana
waheshimiwa kwa kuwa kanisani ni sehemu ya kumwabudu na
kumshukuru Mungu pekee.
“Sisi hatuna vyama ila watu wetu ndio wanavyama na hapa
tunakuja ibadani unajua kilemba au jezi inaashiria chama Fulani sasa hizo ziwe
huko mtaani lakini kwenye ibada tuvae mavazi ya ibada”alisema Lyosi Mwalyosi
“Hata wale wanao fanya
mnada wakisema ni kumheshimiwa Fulani hao ni waheshimiwa huko kwenye majukwaa
yao na hapa wanakuja kama waumini wa kawaida”alisema tena Lyosi Mwalyosi
Aidha amewataka wagombea wote kunadi sera zao pasipo kutumia
lugha za kuchafuana na kuwaomba wananchi kusikiliza sera za wagombea ili
wawapime na wajue ni yupi watakayemchagua.
Baadhi ya wanasiasa ambao wanaabudu katika kanisa hilo
akiwemo Navy Sanga Mgombea wa udiwani kata ya kitisi kupitia CCM
na Seth Vegulla mgombea udiwani kupitia chama
cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamemshukuru mchungaji kwa
kuzuia hayo na kueleza kuwa endapo yangeachwa
yangepeleka mgawanyiko ndani ya kanisa hilo.
“Pale kanisani hatuendi kwa ajili ya uheshmiwa wala hatuendi
kwa ajili ya siasa tunaenda kumshukuru Mungu lazima tuheshimu mahala pa Ibada”
alisema Navy Sanga
Seth Vegulla alisema “Mchungaji
amefanya vizuri sana kwasababu siasa ina nguvu na inaweza kuligawa kanisa”
0 Comments