TANGAZA NASI

header ads

Tamwa yawajengea uwezo wajasiriamali

 


Imelezwa kuwa uboreshwaji wa bidhaa zitokanazo na wajasiriamali visiwani Zanzibar ni moja miongoni mwa njia muhimu zitakazowawezesha wajasiriamali visiwani hapa kuweza kuongeza soko la bidhaa zao kitaifa na kimataifa.

Kauli hio imetolewa na Afisa uwezeshaji wanawake kiuchumi kutoka Tamwa-Zanzibar Nairat Abdalla Ally katika  mafunzo maalumu ya siku moja yenye lengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali hao katika uboreshaji wa vifungashio kwenye bidhaa zao mbali mbali.

Alisema mafunzo hayo yamewashirikisha wajasiriamali 30 kutoka shehia 12 za Unguja kwa lengo la kuwakomboa wanawake katika dimbwi la umasikini na kuondokana na utegemezi kwenye familia zao.

Alisema kwa miaka mingi Zanzibar wapo wajasiriamali ambao wameamka na wenye  kujishughulisha na kazi mbali mbali za uzalishaji wa bidhaa lakini wamekua wakikabiliana na chnagamoto za hapa na pale hususani ubora wa bidhaa zao jambo ambalo alisema wanahitaji kusaidiwa.

‘’Tunaamini kuwa mafunzo haya ya vifungashio kwa wajasiriamali hawa 30 yataleta tija na kufungua milango zaidi ya kibiashara ndani na nje ya Nchi’’aliongezea.

Sambamba na hayo Afisa huyo alitoa wito kwa wajasiriamali walionufaika na mafunzo hayo ya siku moja kuhakikisha wanayafanyia kazi ipasavyo ili yaweze kuleta tija kwao na familia zao.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka taasisi ya Mboga na Matunda Sanje Lufwelo alisema utolewaji wa amfunzo ya vifungashio kwa wajasiriamali ni jambo muhimu kwa wakati huu ambao kuna ushindani mkubwa wa bidhaa za wajasiriamali.

Alieleza kuwa ili bidhaa iwe bora inahitaji mpangilio   hususani kwenye muonekano kabla ya kuanza kwa matumizi ya bidhaa hizo kwa wateja.

‘’Kikawaida mteja huvutiwa na muonekano kabla ya kupata ladha ya kilichomo ndani hivyo unapofeli kwenye kuweka bidhaa zako katika kifungashio bora ni wazi kuwa utawakosa wateja na kushindwa kupiga hatua za kimaendeleo zao’’aliongezea.

Baadhi ya wajasiriamali hao walisema wanamatumaini makubwa na mafunzo hayo nakwamba watayafanyia kazi ipasavyo ili waweze kupata tija.

Post a Comment

0 Comments