TANGAZA NASI

header ads

Rais wa Hungary asema EU yapaswa kubatilisha vikwazo dhidi ya Urusi

 


Rais wa Hungary Viktor Orban amesema kuwa Umoja wa Ulaya unapaswa kubatilisha vikwazo vyake kwa Urusi huku akishinikiza kuanza tena kwabiashara na Urusi na jeshi la Ulaya ambalo linaweza kukabiliana na nguvu za kijeshi za Urusi.

 Kuhusu iwapo Umoja wa Ulaya unapaswa kuiadhibu Urusi kuhusiana na tukio la kulishwa sumu kiongozi wa upinzani nchini humo Alexei Navalny, Orban ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kutokana na mtazamo wa Hungary, hawaoni sababu ya kuchukuwa hatua hiyo lakini iwapo Umoja wa Ulaya utataka kuchukuwa hatua hiyo, basi wako tayari kuitafakari. 

Umoja wa Ulaya uliweka vikwazo dhidi ya Urusi baada ya kulikalia eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine. 

Baadaye ukaviimarisha kufuatia hatua ya Urusi kuwaunga mkono waasi waliokuwa wakikabiliana na vikosi vya serikali Mashariki mwa Ukraine, mzozo ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 13 kufikia sasa.

Post a Comment

0 Comments