Rais wa Guinea, Alpha Condé,amekubali hatua ya chama chake kumteua kugombae muhula tata wa tatu madarakani.
Bw. Condé, ambaye mwanazo alichaguliwa 2010,alishinikiza marekebisho ya katiba kupitia kura ya maoni iliyomwezesha kugombea muhula wa tatu.
Kura hiyo ya maoni ilisusiwa na upinzani katiika hatua amabyo pia ilitibua maandamano.
Mapema mwezi Agosti chama tawala nchini Guinea kilimuidhinisha rais huyo wa miaka 82 kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa Oktoba, lakini ameamua sasa kutoa kauli rasmi kuhusu hatua hiyo.
Juhudi zake za kusalia madarakani zimeibua wasiwasi Guinea huenda akajiiunga nan a nchi zingine za Kiafrika ambazo watawala wake wamekataa kuachia madarakani baada ya mamlaka yao kumalizika.
0 Comments