Na Amiri Kilgalila,Njombe
Katika hali isiyo ya
kawaida mwanafunzi wa shule ya sekondari Madilu iliyopo wilayani ludewa mkoani
Njombe wa kidato cha kwanza Roida Mwabena,amejikuta katika wakati mgumu
mara baada ya sare ya shule aliyovaa kuanza kuungua moto wakati akiwa njiani
kuelekea shuleni ,huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.
Roida Mwabena mtoto aliyekumbwa
na kadhia hiyo anasema alishangaa ghafla kuona moto mkubwa unawake kwenye
mavazi yake na kuamua kuamu kukimbia akirudi kwa baba yake mkubwa.
“Mimi niliona moto unawake
nikarudi nakimbia kwa baba mkubwa akanitoa sketi akauzima ule moto”alisema moto
Roida Mwabena
Mwalimu mkuu wa shule
hiyo Bw.Michael Mwalongo amesema tukio hilo limemkuta mwanafunzi majira ya saa
kumi na mbili asubuhi kwani mtoto huyo amekuwa akitokea nyumbani kulingana na
hali yake ya afya huku baadhi ya wanafunzi wengine wakiishi hosteli.
“Mtoto akiwa njiani
ndio tukio hilo limemkuta,hivyo ameungua sketi ya shule na sweta moto ule wasamalia
wema walijaribu kuuzima na baadaye wakamleta shule,kumchunguza akawa ameungua
na mkono baada ya hapo mzazi akaja kumchukua na piki piki na kumpeleka kituo
cha afya”alisema Michael Mwalongo
Kwa upande wake mganga
mkuu wa kituo cha afya madilu,Salmini magunja amekiri kumpokea mwanafunzi
huyo ambaye alifikishwa zahanati kwa ajili ya matibabu huku nguo zake zikiwa
zimeungu pamoja na mwanafunzi kuwa na majeraha ya moto.
“Tulimpokea na kweli
na yunifomu zilikuwa zimeungua moto na yeye kuna baadhi ya maeneo ya mwili
kidogo ulishika moto,tulimuuliza labda ulitembea na kiberiti alisema hapana,na
hapa tumempa matibabu ya kawaida kama mtu aliyeungua moto japo hili ni jambo la
ajabu mpaka ndugu zake wameshangaa,lakini kwasababu hali yake ni nzuri
tumemruhusu aende nyumbani”alisema Salmini Magunja
Kutokana na hali kituo
hiki kimemtafuta baba mzazi wa mtoto huyo Andrea Mwabena ambaye amekiri mtoto
wake kukumbwa na tatizo hilo la kustaajabisha.
“Tukio limemkuta mtoto
asubuhi,na sisi tunashangaa kwa kweli ndio maana tumekaa tuangalie nini chanzo
cha huu moto,kwasababu moto ukianza kuwaka bila chanzo ni tatizo na ukiangali
hili tukio la moto ni la kwanza hatujawahi kuona”alisema Andrea Mwabena baba wa
mtoto huyo
“Yaani na mimi
silielewi hili tatizo mpaka saizi kwa motto aliaga vizuri asubuhi akaondoka
lakini nikaona baba ake ananipigia simu anasema mama njoo huku moto anawaka
moto”alisema Regina Mnyanga mama wa mtoto
Vile vile mwalimu mkuu
wa shule ya sekondari Madilu amesema tukio la aina hiyo limekuwa la kwanza
kutokea katika shle hiyo licha ya kuwepo kwa matukio mengine ya ajabu kama
watoto kuzimia.
“Hili ni tukio limetushangaza
lakini alikuwa akizimia mara kwa mara,na hili la kupoteza fahamu siku mbili
mpaka tatu ni kawaida lakini hili la moto tumeshangaa”alisema mwalimu Michael Mwalongo
0 Comments