TANGAZA NASI

header ads

Dk Shein awaomba haya wananchama wa CCM

 


NA Thabit Madai,Zanzibar.    

MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja kuhakikisha wanakipatia ushindi wa kishindo chama hicho.

DK.Shein amesema kwamba Chama cha Mapinduzi CCM kimajitahidi katika kuletea maendeleo ya Zanzibar hivyo wasibababushwe na wapinzani wa chama hicho na  wajidhatiti katika kukipatia ushindi chama hicho kiweze kuendelea kuleta maendeleo na kuwakwamua wazanzibar.

Hayo ameyaeleza leo katika Mkutano Mkuu wa hadhara wa kumnadi Mgombea wa Urais wa Zanzibar DK. Hussein Mwinyi pamoja na wagombea w nafai mbalimbali kupitia chama hicho cha Mapinduzi ya Zanzibar, Mkutano huo wa Hadhara umefanyika katika kiwanja cha Shule ya Nungwi alimaarufu kiwanja cha Mapara,Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Dk. Shein alisema Wanachama wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja wanatakiwa kuwa pamoja na kuhakikisa kwamba chama icho kinapata usindi wa kishindo kwa wagombea wake uanzia ngazi ya Urais,Uwakilishi,Ubunge na Udiwani.

Alisema chama cha Mapinduzi tayari kimeshafanya mambo mbalimbali kkatika kuleta maendeleo ya Zanzibar na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo jitihada zao zitasaidia katika kuendeleza pale walipoishia.

“Nataka kuwaambia kuwa Chagueni viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM ambao wanasifa ya kuongoza na kuwatumikia wananchi na msibabaishwe na hao wengine”Alisema Dk.Shein.

Katika Maelezo yake DK.Shein alisema Chama cha Mapinduzi CCM kinaendelea kutimiza nyenzo muhimu zilizotokana na Afro Shiraz Party kwa kuwaunganisha wananchi pamoja na kuwaletea maendeleo.

“Nyenzo hizo muhimu ndio zilizozingatiwa katika kutengeneza Ilani ya Chama chetu kwa mwaka wa 2020/2025 ambapo kuna fikra za kukuza uchumi wetu na kupambanan na Umasikin,”alisema Dk. Shein.

Hata hivyo Dk.Shein aliwasisitiza wanachama wa chama hicho kukipati ushindi CCM kutokana na kuendeleza Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 pamoja na kuendeleza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

“Tunakila sababu ya kutaka kushinda kutokana kwamba Tunataka kuendeleza Mapinduzi pamoja na kuendeleza Muungano wetu wa Serikali mbali, pia kuendeleza Amani umoja na Mashirikiano baina yetu,”alisema Dk. Shein.

Aidha DK.Shein alisema kwamba CCM ina kila sababu a kushinda ili uendeleza yale yote mazuri ambayo tayari wameshaanza katika kuleta maeneleo ya Zanzibar.

Mkutano huo wa hadhara umehudhuriwa na maelfu ya Wananchama wa Chama hicho mcho kutoka maeneo mbalimbali ya kisiwa cha Unguja.

Post a Comment

0 Comments