Na Amiri Kilagalila,Njombe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa
Njombe kimewataka wanachama wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kuchagua
viongozi wenye uwezo wa kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Njombe Rose Mayemba
wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea wa ubunge jimbo la Makambako,ambapo amewataka wanachama
na wananchi kwa ujumla kumchagua mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia chama
hicho kwa kuwa ana uwezo wa kuwasilisha na kutatua changamoto zao.
Aidha mwenyekiti amesema chama chake kimejipanga
kushinda katika uchaguzi huo kuanzia ngazi ya Urais,Ubunge na Udiwani katika
maeneo yote ambayo wamesimamisha wagombea.
“Tuleteeni mtu ambaye akienda kupaza sauti kule huku
utakuta maji yanatanda,na mchagueni General Kaduma kwasababu ana ajenda za
Makambako na ajenda za kitaifa”alisema Rose Mayemba
Naye mgombea wa ubunge jimbo la Makambako General Reuben
Kaduma amesema endapo atapata ridhaa kwa wananchi na kuwa mbunge atahakikisha
anawasaidia wananchi katika kutatua changamoto zinazowakabili katika sekta ya
kilimo,afya,maji na elimu.
“Dhamira nikuwaletea heshima na maendeleo Makambako,watu
wanahusika kwenye biashara,kilimo lakini manufaa ni madogo,nimeona niweze
kuwatumikia wanamakambako ili tuweze kusonga mbele”alisema General Reuben Kaduma
Hata hivyo baadhi ya wagombea wa udiwani kupiti
chama hicho Akiwemo mgombea udiwani kata ya Makambako Daud Tweve,Mgombea
udiwani kata ya kivavi, Baraka Kivambe,mgombe
udiwani kata ya mwembetogwa Sillas Makweta na mgombea udiwani kata ya kitisi Seth
Vegulla wamewaomba wananchi kuwapatia kura zao kwa kuwa wana agenda za
kimaendeleo katika kata hizo.
Tayari tume ya Taifa ya uchaguzi NEC ilishatangaza kuanza
kampeni kuanzia Agosti 26 mwaka huu na vyama vya siasa vinaendelea na kampeni hizo
kwa ajili ya kuendelea na uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu.
0 Comments