Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Taasi binafsi na za Umma
wilayani Njombe zimetakiwa kuketi katika meza ya majadiliano katika masuala ya
kibiashara na kiuchumi badala ya kila sekta kufanya mambo yake.
Katika ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa baraza
la biashara wilaya ya Njombe mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni mkuu wa wilaya
ya Njombe Ruth Msafiri amesema kuwa mkutano huo ni muhimu na kiungo kikubwa cha
uchumi kwa wananchi kwa kufanya majadiliano ya pamoja juu ya changamoto
zilizopo.
“Tuna mambo mengi sana Njombe ambayo tunaweza
kuyafanya lakini sekta binafsi iko peke yake na sekta ya umma iko peke
yake,watu wa Njombe ni hodari wa kufanya kazi sasa tumekutana ili tubadilike na
tuwe wa moja kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika wilaya yetu”alisema
Ruth Msafiri
Mgeni wa heshima katika ufunguzi wa mkutano wa
baraza hilo ni katibu mtendaji wa baraza la biashara taifa Dokta,Godwin Wanga
ambaye amesema hakuna uchumi imara pasina mashirikiano baina ya sekta binafsi
na umma na katika kufanikisha hilo lazima kuwepo kwa majadiliano.
“Mnaweza msijatambue lakini watu wa Njombe
mnatoa mchango mkubwa sana katika taifa letu kupitia kilimo na mna mazao ambayo
yanatusaidia sana hata kuingiza fedha za kigeni,mfano Mbao”alisema Dkt,Godwin Wanga
Awali katibu mtendaji wa chama cha
wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo TCCIA mkoa wa Njombe bwana Leo Tamambele
amesema kuwa vikao vya baraza la biashara husaidia sana kukuza uchumi ndani ya
wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.
“Kwa kweli tunajiskia amani sana na tunaahidi
kufanya kazi kwa bidii kupitia baraza hili” alisema Leo Tamaambele
0 Comments