TANGAZA NASI

header ads

WANANCHI KATA YA KIBASUKA WALALAMIKIA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA SALAMA.


Na Mwandishi wetu Tarime.

Wananchi kata ya Kibasuka wilayani Tarime mkoani Mara wanalazimika kuchota maji ya mtaro kando kando ya barabara kutokana na kutembea mwendo mrefu kutafuta huduma ya  maji ya  bomba jambo ambalo linasababisha  baadhi ya familia kusambaratika.

Wakiongea na  Dar mpya blog wananchi hao wamedai kuwa wanalazimika kutumia maji ya  mtaro  pale mvua zinapokuwa zimenyesha kutokana na ukosefu wa maji safi na salama na umbali mrefu ili kupata maji safi na salama.

 “Hapa kijijini kwetu weigita kata ya kibasuka wanawake tunalazimika kutembea umbali mrefu pia kutembea usiku kwa ajili ya kutafuta maji safi na salama na wakati mwingine tunachelewa na wanaume wanalazimika kutupiga na wengine ndoa kuachika”  alisema Beatrice.

Pia Suzana Marwa ambaye ni mkazi wa kata ya Kibasuka  aliongeza kuwa wamekuwa wakijengewa visima na wadau wa maendeleo pamoja na serikali na kushindwa kudumu kwa muda mrefu jambo ambalo hufanya tatizo hilo kuendelea kuwa sugu kijijini hapo.

Hivyo wameiomba serikali kuingilia kati kwa ajili ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa kuchinbiwa visima virefu kwani maji yanayotumika siyo rafiki kwa ajili ya afya zao.

“Maji haya watoto wanawezakuugua vichocho pamoja na matumbo kwa sababu pia mifugo inatumia maji haya ambayo umeona tunachota baada ya mvua kunyesha hivyo wakati wa kiangazi tunateseka sana.

  Wananchi hao wameongeza kuwa wakati wa kiangazi wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwa ajili ya kufuata huduma ya maji Jambo ambalo linasababisha kwa kwamisha uzalishaji ili kujipatia kipato.

Post a Comment

0 Comments